Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aishi, Mwantika waikosa Kenya

68605 Pic+mwantika

Sun, 28 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

NYOTA wawili wa kikosi cha timu ya taifa, 'Taifa Stars', kipa Aishi Manula na beki David Mwantika wataukosa mchezo wa kwanza kufuzu fainali za CHAN, dhidi ya Kenya, 'Harambee Stars', utakaochezwa leo Jumapili saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa.

Kukosekana kwa Manula kunampa nafasi kubwa kwa nahodha msaidizi wa timu hiyo, Juma Kaseja kuanza pambano hilo la leo la kuwania Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani zitakazochezwa mwakani nchini Cameroon.

Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na Ofisa habari wa Shirikisho la soka Tanzania Cliford Ndimbo, inaeleza kuwa wachezaji hao hawatakuwa katika mchezo wa leo jioni dhidi ya Kenya kutokana na majeraha ambayo wameyapata.

"Taarifa zaidi za kitabibu zitafata kueleza aina ya majeraha ambayo waliyapata wachezaji hao mpaka kushindwa kuwa sehemu ya kikosi cha Stars ambacho kitacheza dhidi ya Kenya," alisema Ndimbo.

Manula na Mwantika wanaungana na Mudathir Yahya ambaye nae alishindwa kujiunga na kikosi hikob kutokana na majeraha ambayo aliyapata kabla ya kuitwa katika timu na Kaimu kocha mkuu wa Stars Ettiene Ndayiragije.

Stars wanacheza mchezo huo wa kufuzu CHAN, ambayo itafanyika nchini Cameroon, mwakani huku mechi ya marudiano na Kenya itakuwa Agosti 4, ambayo itachezwa pale Nairobi.

Pia Soma

Ikumbukwe kama Stars itafanikiwa kuondoka na ushindi katika mchezo huo itakutana na Sudan katika hatua inayofuata.

Chanzo: mwananchi.co.tz