Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

African Lyon yaliza mtu huko

Lyon Pic Data African Lyon yaliza mtu huko

Mon, 12 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KLABU ya African Lyon inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza, jana ilipata ushindi wa 3-1 dhidi ya Boma Fc mchezo wa kundi A uliochezwa katika uwanja wa Uhuru, Dar.

Ushindi huo unawafanya Lyon washike nafasi ya nne katika msimamo wa kundi huku wakiwa na pointi 17 katika mechi 13 walizocheza mpaka sasa.

Lyon ambayo kwasasa inanolewa na kocha Khalid Adam, amepanga kuhakikisha timu hiyo inakaa katika sehemu nzuri kwenye msimamo wa kundi A.

"Naiona timu ikiwa katika sehemu nzuri, huku chini wachezaji inabidi uwajenge kisaikolojia kwa sababu hakuna pesa, lakini kama tukifanya vizuri huko mbele watapata pesa".

Mechi zingine za kundi A zilizochezwa ni Njombe Mji1-1 Majimaji FC, Ken Gold 0-2 Mbeya Kwanza na African Sports 1-0 Mawenzi Market.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz