Dar es Salaam. Aliyekuwa afisa habari wa Simba SC na mwandishi wa habari za michezo, Asha Muhaji amefariki dunia mchana wa leo, Jumatano.
Asha (50) amekutwa na mauti wakati anaendelea na matibabu hospitali ya Hindu Mandali iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mdogo wa marehemu, Habibu Kaumo alithibitisha kifo cha dada yake kuwa kilitokana na kusumbulia na TB ya ngozi iliyogundulika baada ya kufanyiwa vipimo juzi Jumanne.
Alisema kuwa marehemu mara kadhaa alikuwa akiumwa, lakini tatizo hilo halikugundulika hadi alipopelekwa katika hospitali hiyo ambako alilazwa tangu Alhamisi ya wiki iliyopita.
"Alikuwa anaumwa na mwili wake ulikuwa ukidhoofika kadri siku zinavyokwenda bila kujua tatizo kuwa ni TB ya ngozi ambayo awali haikujulikana kama anayo," alisema na kuongeza
"Baada ya vipimo ndipo amegundulika kuwa ana tatizo hilo lakini akiwa katika hali mbaya sana ya kupumulia mashine, madaktari wamejitahidi kadri ya uwezo wake, lakini Mungu ameamua kumpumzisha mchana wa leo." alisema
Pia Soma
- Barua nzito ya GSM kwa Yanga yaleta utata
- Usajili wa Morrison waibua utata Yanga
- Mwisho wa enzi! Yondani akili inataka mwili unagoma
"Tumeutoa mwili hospitalini na kwenda kuuhifadhi msikiti wa Mahmuru uliopo Upanga ambapo kesho leo atafanyiwa ibada kabla ya kuelekea makaburi kumpumzisha, marehemu hajaacha mtoto" alisema
Asha enzi za uhai wake aliwahi kufanyakazi kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo Uhuru na New Habari akiwa mhariri wa michezo gazeti la Rai.