Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afariki kwenye riadha

Riadha Mauaji Afariki kwenye riadha

Tue, 4 Oct 2022 Chanzo: Radio Jambo

Mwanaume mwenye umri wa miaka 36 alifariki baada ya kuzimia alipokuwa akikimbia mbio za London Marathon, waandalizi wamethibitisha.

Mwanaume huyo, kutoka kusini-mashariki mwa Uingereza, aliugua kati ya maili 23 na 24 kati ya tukio la maili 26.2.

Alipata matibabu ya haraka na gari ya wagonjwa ilifika ndani ya dakika tatu lakini alifariki baadaye hospitalini. Chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana.

Katika taarifa yake, waandaaji wa London Marathon walisema "wanatoa pole za dhati" kwa familia na marafiki wa mtu huyo.

Shirika hilo lilisema jamaa zake walikuwa wameomba faragha wakati huu, na kuongeza:

"Hakuna maelezo zaidi yatatolewa kwa mujibu wa matakwa yao. "Sababu ya kifo itajulikana baadaye kupitia uchunguzi wa matibabu."

Chanzo: Radio Jambo