Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adhabu mavazi ya Zahera utata mtupu

74356 Zaheraa1+pic

Thu, 5 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mavazi nadhifu na ya heshima ni yapi? Ndio mjadala ulioibuka kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram na Twitter baada ya kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kupigwa faini ya Sh 500,000 kwa kuvaa mavazi yasiyo nadhifu na ya heshima wakati wa mechi.

Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imempiga faini ya Sh 500,000 Zahera kwa kuvaa mavazi yasiyo nadhifu na ya heshima katika mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara msimu huu dhidi ya Ruvu Shooting iliyofanyika Agosti 28 mwaka huu kinyume cha Kanuni ya 14(2m) ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za Mchezo.

Kanuni hiyo ya 14(2m) inasema: “Kocha mkuu na viongozi wa benchi la ufundi wanawajibika kuvaa sare maalum za timu yao kwa benchi la ufundi. Endapo kocha mkuu atahitaji kuvaa mavazi tofauti, anawajibika kuwa katika mavazi ya heshima na nadhifu. Ukiukwaji wowote utavutia adhabu kwa mhusika na / au kwa timu husika.” Mwisho wa nukuu.

Kwenye mitandao ni moto

Baada ya taarifa hizo za kocha Zahera kupigwa faini, mijadala mikubwa ikaibuka kwenye mitandao ya kijamii wengine wakisema ameonewa na wengine wakisema ni sahihi kwa Bodi ya Ligi kumpiga faini.

Mjadala mkubwa huko ni swaii ‘mavazi ya heshima na nadhifu ni yapi?’ Wengine wanamtetea Zahera kuwa hata kama anapenda kuvaa kaptula fupi na tisheti na chini bado yuko nadhifu na wengine wakisema ‘hapana hawi nadhifu’.

Pia Soma

Advertisement
Baadhi ya watu walikuwa wakituma picha za makocha wa timu kubwa ulimwenguni kama kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson na kocha wa Mancheter City, Pep Guardiola ambazo walikuwa wamevaa mavazi tofauti tofauti.

Ferguson alionekana kuvaa kaptura fupi nyeusi na tisheti nyeupe zote zikwia na nembo ya Manchester United akiwa pamoja na wenzake kwenye benchi la ufundi hivyo watu kutoa maoni yao katika picha hiyo wengine wakisema alikuwa katika mavazi sahihi na wengine wakipinga wakisema katika picha hiyo alikuwa mazoezini na si katika mechi.

Kocha Mwinyi Zahera amesema anashangazwa na kupigwa faini eti kwa sababu ya kuvaa mavazi yasiyo na heshima huku akidai mtu anayekosa heshima ni yule anayeidharau Yanga.

“Wanasema vile ninavyovaa mimi nawakosea watu heshima lakini lazima wajue mtoto wa mfalme wa Monaco ya Ufaransa anavaa hivi (kama yeye Zahera), mtoto wa mfalme wa Uingereza, Prince Harry anavaa hivi, kukosea watu heshima ni kudharau Yanga kwani ni timu kubwa. Kama Yanga mnaidharau mnaionea, hiyo ndio kukosa heshima.

“Siku ya hizo mechi na Ruvu Shooting saa 6:30 mchana ndipo wale waliotoka kwenye kikao cha maandalizi ya mechi wakaniambia kocha wanasema leo huwezi kuvaa kaptula nikawajibu sasa nifanyeje maana tumetoka Botswana tukafikia moja kwa moja kambini na mpaka sasa sijaiona nyumba yangu na saa 7:45 tunatakiwa kwenda uwanjani, nitoke niende kutafuta nguo ya kuvaa halafu nirudi tena kambini ndio twende uwanjani ingewezekanaje?”

Alipoulizwa Zahera baada ya adhabu hiyo je atabadili aina yake ya uvaaji alijibu kwa kifupi “waulize wenyewe”.

Akiongelea kuhusu kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kutoa shutuma na kejeli kwa Bodi ya Ligi, Zahera alijibu kuwa haoni kosa lake kwani alifanya kwa faida ya soka la Tanzania.

Aidha, aiisema kufungiwa kwake mechi tatu hakutaathiri kikosi chake kwani kocha msaidizi wake wapo.

Chanzo: mwananchi.co.tz