Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Achana na bao la Chama watazame wababe wanaoisubiri Simba

33348 Pic+simba Tanzania Web Photo

Wed, 26 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bao la dakika za majeruhi lililofungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Simba, Mzambia Cleotous Chama yawezekana ni bao muhimu zaidi kwa takribani misimu mitano iliyopita ndani ya klabu hiyo.

Sio uzuri wake tu kwa kuwa wenye soka lao hususani vijana wanasema bao hilo la kisigino ni la kideoni, bali hata lilivyoweza kuamua hatima ya Simba kuandika historia nyingine kwa kuwa klabu ya kwanza Tanzania kuingia kwa mara ya pili katika hatua ya timu 16 bora zinazowania klabu bingwa Afrika.

Awali Simba ilitinga katika hatua kama hiyo mwaka 2003 ilipokitoa kigogo cha soka Afrika timu ya Zamalek ya Misri.

Si hivyo tu, Simba imejiongezea rekodi bora Tanzania na Afrika Mashariki baada ya ile iliyotangulia mwaka 1993 ilipotinga katika fainali za kombe la CAF (sasa kombe la shirikisho) na kutolewa katika ardhi ya Tanzania kwa kufungwa magoli mawili kwa moja na klabu ya Stellar Abidjan ya Ivory Coast. Rekodi hiyo haijawahi kufikiwa na timu nyingine yoyote Afrika Mashariki.

Hata hivyo, ushindi huo wa Simba unamaanisha kwamba sasa inakwenda kukutana na timu kali zaidi na vigogo vya Afrika ambazo zina uzoefu mkubwa na zilizojidhatiti kwa kuwekeza vya kutosha.

Tayari timu zote zitakazoumana katika hatua ya makundi zimeshafahamika na hapa tunakuletea kwa uchache kuhusu miamba hiyo yenye historia kubwa.

Al Ahly SC (Misri)

Hiki ni kigogo cha Soka Afrika kikiwa na makao yake Cairo, Misri.

Ilianzishwa Aprili 24, 1907, jijini Cairo ni miongoni mwa timu zenye historia kubwa katika soka Afrika kwani imewahi kulibeba kombe hilo mara kadhaa.

TP Mazembe

Makao makuu yake yapo mjini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC). Inatajwa kuwa timu yenye mafanikio makubwa Afrika huku hatua kubwa zaidi iliyowahi kufikia mbali na kuchukua ubingwa wa klabu bingwa Afrika ni kuifunga timu ya International ya Brazil katika nusu fainali kuwania klabu bingwa ya dunia mwaka 2010.

=Ismailia (Misri)

Waarabu wenyewe wanaiita El-Nady El-Ismaily. Ilianzishwa Aprili 13, 1924 ikijulikana kama El Nahda Sporting Club.

Klabu hiyo ambayo kwa utani imebatizwa jina la The Brazilians, inatajwa kuwa kipenzi cha Wamisri kutokana na mchango wake katika mafanikio ya wachezaji wengi hususani wazawa.

Ndiyo timu ya kwanza kutoka nchini humo kutwaa ubingwa wa klabu bingwa Afrika mwaka 1969.

Mwaka 2003 ilitinga fainali ya michuoano hiyo na kupoteza kwa Enyimba ya Nigeria, ambayo katika hatua za makundi mwaka huo ilikuwa kundi moja na Simba.

Whydad Casablanca (Morocco)

Ilianzishwa Mei, 1937 mjini Casablanca ikifahamika kama Wydad Athletic Club.

Mechi za nyumbani hutumia uwanja wake wa Stade Mohammed V.

Ina rekodi ya kuzoa makombe kibao tangu ilipoanzishwa ikiwemo kubeba mara mbili klabu bingwa Afrika, Kombe la Washindi (sasa Shirikisho), klabu bingwa kwa nchi za kiarabu na klabu bingwa kwa nchi za Afrika Kaskazini.

Esperance (Tunisia)

Jina lake kamili ni Esperance Sportive de Tunis. Ilianzishwa Januari 15, 1919, mechi zake za nyumbani hutumia dimba la Stade Olympique de Rades Tunis, Tunisia

Ndio klabu maarufu na yenye mashabiki wengi nchini Tunisia.

Imefanikiwa kutwaa kombe la klabu bingwa kwa nchi za kiarabu huku mara mbili wakimaliza nafasi ya pili. Imewahi kutwaa klabu bingwa Afrika mara tatu, kombe la washindi Afrika, kombe la CAF na taji la klabu bingwa Afrika Kaskazini.

Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)

Ikitumia rangi ya njano, Mamelodi Sundown Football Club ilianzishwa mwaka 1970, mjini Pretoria.

Mechi zake za nyumbani hucheza katika uwanja wa Lucas Masterpieces Moripe wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 28,900 na Loftus Versfeld Studium unaoingiza watu 51,762.

Mwaka 2016 ilitwaa ubingwa wa klabu bingwa Afrika na ina rekodi ya kuwa klabu ya kwanza Afrika Kusini kushiriki michuano ya klabu bingwa ya dunia na kumaliza nafasi ya sita.

Orlando Pirates F.C. (Afrika Kusini)

Ilianzishwa mwaka 1937 ikijulikana kama Orlando Boys Club. Mwaka 1995 ilitwaa taji la klabu bingwa Afrika na hadi sasa ni wao na Mamelodi pekee ndizo timu zilizofanikiwa kutwaa taji hilo kutoka Afrika Kusini.

CS Constantine (Algeria)

Ilianzishwa Juni 26, 1898, mechi zake za nyumbani hucheza katika uwanja wa Stade Mohemed Hamloud unaoingiza watu 45,000.

Haijawahi kutwaa taji lolote kati ya yale yanayoandaliwa na CAF.

Lobi Stars (Nigeria)

Ni klabu changa ikilingashwa na Simba kwani ilianzishwa mwaka 1981, lakini imeshiriki michuano ya klabu bingwa Afrika mara moja na kombe la shirikisho mara tatu.

FC Platnum (Zimbabwe)

Klabu hiyo ilianzishwa mwaka 1995, hata hivyo imewahi kushiriki mashindano ya klabu bingwa Afrika mara tatu na kombe la shirikisho mara moja ingawa mara zote iliishia hatua za awali.

Asec Mimosa (Ivory Coast)

Jina lake kamili ni Association Sportive des Employés de Commerce Mimosas

Ilianzishwa mwaka 1948 na imeshiriki michuano ya klabu bingwa Afrika mara 13 na kufanikiwa kutwaa kombe hilo mara moja na shirikisho mara 12.

JS Saoura (Algeria)

Klabu hiyo hiyo iliyoanzishwa mwaka 2008 imeshiriki mara moja tu michuano ya klabu bingwa Afrika.

AS Vita (DRC)

Hii ilianzishwa mwaka 1935.



Chanzo: mwananchi.co.tz