Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Abreu, kiboko ya Anelka aliyevunja rekodi duniani

9248 PIC+REKOD TanzaniaWeb

Wed, 1 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Wakati wengi wakimfahamu mshambuliaji nguli wa zamani wa Chelsea, Nicolas Anelka ndiye mchezaji aliyezitumikia klabu nyingi duniani, wanakosea.

Yupo mchezaji asiyekuwa na jina kubwa duniani, Sebastian Abreu raia wa Uruguay ndiye anayeshika rekodi ya kuzitumikia klabu nyingi duniani.

Anelka aliyezoeleka na muonekano wa upara kichwani amepita kwenye klabu 14 tofauti duniani akijumuisha na akademi tatu kabla ya mwaka 1996 kupandishwa kikosi cha kwanza Paris Saint-Germain.

Abreu aliyezaliwa Minas mjini Lavalleja, Urugaay amemzidi mara mbili Anelka kwa klabu alizocheza akiwa na umri wa miaka 41, lakini bado anapambana.

Nyota huyo wa klabu ya Deportes Magallanes inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Chile maarufu ‘Primera B de Chile’. Mpaka sasa mkongwe huyo amezitumikia klabu 25 katika nchi 11 tofauti duniani.

San Lorenzo (Argentina), 1996-1998 na 2000-2001 (mkopo), Deportivo La Coruna (Spain), 1998-2004 Gremio (Brazil), 1998 (mkopo), Estudiantes Tecos (Mexico), 1999-2000 (mkopo) na 2004 (mkopo), Club Nacional (Uruguay), 2001 (mkopo), 2004-2005, 2013-2015, Cruz Azul (Mexico), 2002-2003 (mkopo).

America (Mexico), 2003 (mkopo), Dorados de Sinaloa (Mexico), 2005-2006, Monterrey (Mexico), 2006, San Luis (Mexico), 2007, Tigres UANL (Mexico), 2007, River Plate (Argentina), 2008 (mkopo) na 2008-2009, Beitar Jerusalem (Israel), 2008, Real Sociedad (Spain), 2009 (mkopo).

Aris Thessaloniki (Greece), 2009-2010 Botafogo Rio De Janeiro (Brazil), 2010-2012, Figueirense (Brazil), 2012 (mkopo), Rosario Central (Argentina), 2013-2014 (mkopo), SD Aucas (Ecuador), 2015 (mkopo), Sol de America (Paraguay), 2016, Santa Tecla (El Salvador), 2016.

Bangu Atletico Clube (Brazil), 2017 Central Espanol (Uruguay), 2017, Puerto Montt (Chile), 2017, Audax Club Sportivo Italiano (Chile), 2018.

Ngazi ya timu ya Taifa, Abreu ameichezea Uruguay mara 70, ikiwemo mwaka 2002 na 2010 katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Japan/South Korea na Afrika Kusini.

Chanzo: mwananchi.co.tz