Orodha ya mwanamichezo bora wa mwaka 2021 imetangazwa. Wanamichezo sita wamechaguliwa na jopo la wanahabari kutoka Afrika na nchini Uingereza. Jopo hilo limechagua orodha hiyo kutokana na mafanikio katika michezo yao katika jukwaa la kimataifa mwaka 2021 kati ya mwezi Januari hadi Septemba.
Uwezo na mafanikio ya mtu zaidi ya mchezo wao maalum pia ulizingatiwa.
Walioteuliwa ni:
1. Eliud Kipchoge (Mwanariadha)
2. Faith Kipyegon (Mwanariadha)
3. Ntando Mahlangu (Mwanariadha mlemavu)
4. Christine Mboma (Mwanariadha)
5. Edouard Mendy (Mwanasoka)
6. Tatjana Schoenmaker (Muogeleaji)
7. Unaweza kumpigia kura mshindi.
Mwisho wa kupiga kura ni 11.59 usiku siku ya Jumapili tarehe 19 Desemba na mshindi wa tuzo hiyo atatangazwa siku ya Ijumaa tarehe 7 , Januari 2022 katika runing ya Focus on Africa na radio na katika mtandao wa habari za michezo wa BBC Sport.
Haya hapa ni maelezo zaidi kuhusu wanaowania tuzo hiyo.
Eliud Kipchoge
Eliud Kipchoge alikimbia muda bora zaidi 2019 lakini haiukufanywa kuwa rasmir
Taifa: Kenya Umri: 37Mbio: Mwanariadha wa mbio za Marathon
Anadaiwa kuwa mwanariadha bora zaidi wa mbio za marathon mwaka huu, Eliud Kipchoge aliimarisha hadhi yake zaidi katika maili 26.2 baada ya kushinda dhahabu yake ya pili ya Olimpiki katika mashindano hayo.
Akiwa mtu wa tatu kufanikiwa kutetea taji la Olimpiki , raia huyo wa kenya baadaye alichaguliwa kuwa mwanaraidha bora wa kiume na kamati ya kimatiafa ya michezo ya Olimpiki.
Ushindi wake mjini Tokyo una maana kwamba ameshinda mara 13 kati ya mbio15 za Marathon alizokimbia tangu alipoanza kukimbia mbio hizo 2013 , huku akijiongezea sifa za kuvunja rekodi ya dunia ya 2:01:39 aliyoweka mjini Berlin 2018.
Akiwa na umri wa miaka 36, alikuwa mwanariadha mwenye umri mkubwa zaidi kushinda taji la OIimpiki tangu mwanaraidha wa Ureno Carlos Lopes wakati huo akiwa na umri wa miaka 37 mwaka 1984 na kupata ushindi mkubwa zaidi tangu 1972.
Faith Kipyegon
Taifa: Kenya Umri: 27 Riadha: Mwanariadha wa mbio umbali wa kati
Faith Kipyegon alivunja rekodi ya michezo ya Olimpiki mjini Tokyo alipotetea taji lake la mbio za mita 1500m aliloshinda mjini Rio de Jeniro 2016. Mkenya huyo alitoa ushindi huo kwa bintiye mwenye umri wa miaka mitatu, ambaye anamsifu kwa kumpa motisha zaidi baada ya kuchukua mapumziko ya miezi 21 kutoka kwa mchezo huo.
Kujitolea kwake kulikuwa muhimu zaidi kwani Kipyegon ni mwanariadha wa tatu pekee kuhifadhi taji la Olimpiki baada ya kujifungua kati ya Michezo (pamoja na Shirley Strickland wa Australia, mwaka wa 1956, na Francoise Mbango wa Cameroon, mwaka wa 2008).
Kabla ya onyesho lake huko Japani, alikuwa ameweka muda bora zaidi duniani wa 3:51.07 - mara ya nne kwa kasi zaidi katika historia - na huko Monaco mnamo Julai katika mashindano ya Diamond League, hafla ambayo alitawazwa bingwa wa mwaka huo mnamo Septemba.
Baada ya rekodi yake ya Olimpiki, sasa analenga rekodi ya dunia.
Ntando Mahlangu
Taifa: South AfricaUmri: 19 Riadha: Long jumper na mwanariadha wa mbio za miata 200m
Ntando Mahlangu alishinda medali ya wanariadha walemavu akiwa na umri wa miaka 14 , wakati aliposhinda medali ya fedha katika T42 mita 200 katika michezo ya Olimpiki ya Rio 2016 - miaka miwili tu alipoanza kushiriki mashindano ya mchezo huo.
Mwaka huu , alijiongezea mafanikio wakati alipojishindia medali ya dhahabu katika mbio za mita 200 upande wa wanaume na kuruka long jump (T63) mjini Tokyo. Kuruka kulikomshindia dhahabu kuliweka rekodi ya mita 7.17 licha ya kwamba alianza mazoezi wiki sita kabla ya michezo hiyo.
Akiwa na siku njema zijazo zenye mafanikio katika riadha hiyo ya uwanjani , kutokana na ulemavu wake wa mikono na mwenye unmri wa miaka 10 - alichanganya ufanisi wake wa riadha na elimu yake . Mwezi Aprili alivunja rekodi ya dunia katika mbio za mita 200 upande wa wanaume.
Christine Mboma
Taifa: Namibia Umri: 18 Mchezo: Mbio fupi
"Mbio bora katika maisha yangu " - hivyo ndivyo Christine Mboma alivyoelezea ushindi wake jijini Tokyo Japan 2020 baada ya kuwa mwanamke wa kwanza nchini Namibia kusimama katika jukwa la medali la Olimpiki. Baada ya kulishindia taifa lake medali baada ya miaka 25, kijana huyo alijishindia medali ya fedha katika mbio fupi za mita 200, akimaliza nyuma ya bingwa mara tano wa michezo ya Olimpiki kutoka Jamaica Elaine Thompson Herah. Muda wake wa dakika 21 na sekunde 81 ndio uliokuwa bora zaidi kuwahi kushindwa na mwanamke chini ya umri wa miaka 20.
Baadaye aliibuka mshindi katika mbio za Diamond league mita 200 mwezi Septemba mjini Zurich, ambapo muda wake wa dakika 21 .sekunde 78 ulivunja rekodi nyengine ya dunia na rekodi mpya ya Afrika. Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 18 alianza kulenga mbio za mita 200 mapema mwaka huu, baada ya kuzuiliwa kushiriki katika mbio za mita 400 na shirika la riadha duniani kutokana na kumiliki homoni nyingi za kiume.
Edouard Mendy
Taifa: Senegal Age: 29 Mchezo: Kipa wa soka
Edouard Mendy amevutia wengi katika uwanja wa Stamford Bridge tangu aliposajiliwa na Chelsea kutoka klabu ya Ufaransa ya Rennes mwezi Septemba 2020 na ni miongoni mwa kikosi cha klabu hiyo kilichoshinda kombe la klabu bingwa Ulaya mwezi Mei.
Alifanikiwa kuweka rekodi ya mechi tisa bila kufungwa kabla ya kupata ushindi wa taji hilo katika msimu wake wa kwanza . Mendy pia aliweka historia kwa kuwa kipa wa kwanza Mwafrika kushiriki katika mechi za fainali za klabu bingwa Ulaya na mara ya kwanza katika michuano hiyo tangu kipa wa Zimbabwe Bruce Grobbelaar alipocheza katika fainali ya kombe la Ulaya akiichezea Liverpool.
Mendy alicheza mechi 19 bila kufungwa msimu uliopita katika michunao ya klabu bingwa ligi ya uingereza kabla ya kushinda taji la Uefa la kipa bora msimu wa 2020-21.
Mshindi huyo wa Uefa supercup pia ameteuliwa kuwania taji la Fifa la kipa bora 2021, lakini mtu aliyeibuka katika nafasi ya pili katika kombe la FA mwezi Mei , hivi majuzi alishindwa kushinda taji Yshind Trophy kutoka Ufaransa kwa kuwa kipa bora Ulaya.
Tatjana Schoenmaker
Taifa: South Africa Umri: 24 Mchezo: Breaststroke
Tatjana Schoenmaker alijiwekea sifa katika mashindano ya mjini Tokyo ambapo hakushinda dhahabu pekee na fedha akiishindia Afrika Kusini , lakini pia aliweka rekodi ya michezo ya olimpiki katika umbali wa mita 200 na mita 100 mtawalia. Kwa kufanya hivyo , aliishindia Afrika Kusini medali ya kwanza katika uogeleaji upande wa akina dada tangu 2000 na kusitisha subra ya taifa lake la miaka 25 ili kupata medali ya upande wa akina dada katika kidimbwi ambapo alimaliza wa kwanza katika fainali ya mita 200.
Schoenmaker karibu ajiondoe mwaka 2016 baada ya kushindwa kufuzu katika michezo ya Olimpiki ya Rio kwa sekunde cha tu. Lakini aliendelea na mchezo huo na kufikia sasa amejishindia mataji kadhaa ya kimataifa na ya kitaifa , medali mbili za dhahabu katika michezo ya Commonwealth Games pamoja na medali ya fedha. Changamoto inayokuja , ni jinsi ya kujiimarisha mimi binafsi? ''nafurahia kuona ni wapi uogeleaji wangu utaelekea'', alisema.