Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

50 Cent adhamini Timu ya Wanawake

DF SPORT PREVIEW FIDDY 2 50 Cent adhamini Timu ya Wanawake

Tue, 10 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

‘Rapa’ kutoka nchini Marekani 50 Cent amewashitua wengi baada ya kufanya maamuzi ya kuwa mdhamini wa ‘timu’ ya wasichana wenye umri chini ya miaka 14 ya mpira wa miguu kutoka Wales.

‘Timu’ hiyo ya AFC Rumney ilidhaminiwa na mkali huyo kutokana na mmoja wa mzazi wa mchezaji katika ‘timu’ hiyo kufanya kazi na Cent katika ziara yake ya ‘kimuziki’ kwa siku za hivi karibuni ambapo wazazi walimshawishi aongee na mwanamuziki huyo kuhusu kufadhili ‘timu’ hiyo.

Richie Brown ambaye ni ‘meneja’ wa ‘timu’ hiyo kufuatia taarifa yake ameeleza kuwa wachezaji hao wasiwe na hofu maana 50 Cent amekubali kuwadhamini na kufadhili vifaa vya kuchezea.

Hivyo basi wachezaji watavaa ‘jezi’ za ugenini za tracksuit iliyoandikwa G-Unit ambalo ni kundi la muziki wa hip-hop kutoka Marekani, huku chini kidogo ya track hiyo ikiandikwa jina la 50 Cent.. .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live