Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zanzimana nusu mtu nusu sokwe, awashangaza watu anakula majani (+video)

Video Archive
Sat, 19 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

Zanzimana Ellie (21) ni Kijana wa Rwanda ambae amekua gumzo kutokana na utofauti alionao na Binadamu wengine akiwa hana uwezo wa kuongea na muda mwingi anapenda kukaa kwenye Msitu karibu na nyumbani kwao akila majani.

Mama yake mzazi anasema alijifungua Zanzimana baada ya sala yake na Mume wake kumpigia magoti Mungu kuomba awape Mtoto ambae ataishi miaka mingi tofauti na Watoto wao watano wa mwanzo ambao walifariki mmoja baada ya mwingine wakiwa wadogo na hiyo iliwaumiza sana.

Miezi 9 baadae ndio akajifungua Zanzimana ambae pia alikua na kichwa kidogo kuliko Binadamu wa kawaida na sasa anaishi msituni, haongei na hali chakula cha kawaida bali majani na sasa Watalii wanafunga safari kwenda kumtazama.

Chanzo: millardayo.com