Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu ampa wiki moja Prof. Ndalichako

Video Archive
Mon, 10 Aug 2020 Chanzo: millardayo.com

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amempa wiko moja Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Ndalichako, kuhakikisha anakutana na wakuu wa vyuo vikuu nchini, ili kubaini vyuo ambavyo vimeshindwa kuwasilisha mchango wa wanafunzi katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

Ametoa agizo wakati akifungua mkutano mkuu wa kwanza kwa mwaka 2019/2020 wa Jumuiya ya wanafunzi ya Taasisi ya elimu ya juu Tanzania (TAHLISO) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Waziri Mkuu Mjaliwa ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wanafunzi hao yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa TAHLISO Peter Noboye ambaye amesema kwamba kumekuwa na ucheleweshwaji wa vitambulisho vya Bima ya afya unaotokana na baadhi ya vyuo kuchelewesha kufikisha fedha NHIF.

Aidha ameziagiza menejimeti zote za vyuo vikuu nchini kuendelea kushirikiana kwa ukaribu na serikali za wanafunzi kwenye vyuo vyao ili waweze kushughulikia changamoto za wanafunzi kwa wakati.

TAZAMA WALICHOFANYA WAPENZI WA ACT WAZALENDO ZANZIBAR

Chanzo: millardayo.com