Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Warioba: Uchaguzi uwe wa huru na haki

Warioba (2) Jaji Mstaafu Joseph Warioba

Thu, 19 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutokana na umuhimu mkubwa ulionao uchaguzi ujao waserikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024, Jaji mstaafu Joseph Warioba amesema lazima kuhakikishwe unakuwa huru na haki.

Amesisitiza lazima itafutwe njia watu waridhike nao kwa maana ufuate utaratibu ikiwemo wananchi kushiriki kwa wingi kuwachagua viongozi nawatakaoshinda watangazwe kwani uchaguzi huo utakuwa una umuhimu mkubwa kwa amani ya Tanzania,

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Septemba 19, 2024 Jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) JiJini Dar es Salaam unaowakutanisha wadau kujadili tathmini ya hali ya demokrasia nchini.

"Tafadhali viongozi wote wanaohusika lazima tukubaliane tutakapokwenda kwenye uchaguzi tuwe tumekubaliana kwanza, la sivyo tukienda na mapambano haya tuliyonayo inaweza kujenga misingi ya vurugu nchini.

"Mambo ya uchaguzi ndio yanayoanzisha vurugu na yana historia hapa nchini kama vurugu za mwaka 2001, amesema Warioba.

Jaji Warioba aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ametaka makundi yanayovutana hususan viongozi wa vyama vya siasa kukutana na kujadiliana ili kuwa na mwafaka wa pamoja kabla ya kwenda kwenye uchaguzi huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live