Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili Mwasipu: 'Boni Yai' amepelekwa Mahakama ya Kisutu

Boniface Jacob Kisutu Wakili Mwasipu: 'Boni Yai' amepelekwa Mahakama ya Kisutu

Thu, 19 Sep 2024 Chanzo: Mwananchi

Kada wa Chadema na mwanamitandao, Boniface Jacob maarufu ‘Boni Yai’ imeelezwa kuwa amepelekwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Alhamisi Septemba 19, 2024.

Taarifa ya kupelekwa mahakamani huko imetolewa na Wakili wa Chadema, Hekima Mwasipu alipoulizwa na Mwananchi.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime katika taarifa aliyoitoa jana Septemba 18, 2024 alisema jeshi hilo limemkamata na linamshikilia Jacob, mkazi wa Mbezi Msakuzi, jijini Dar es Salaam kutokana na makosa ya kijinai anayotuhumiwa nayo.

Boni Yai alikamatwa Septemba 18, akiwa maeneo ya Sinza, jijini Dar es Salaam, kwa mujibu wa wakili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Hekima Mwasipu anayemwakilisha Jacob.

Awali usiku wa kuamkia leo, Wakili Mwasipu alisema, Jacob anatuhumiwa kwa kosa la kusambaza taarifa za uongo na sababu za kukosa dhamana jana Septemba 18, 2024 mlalamikaji ni makao makuu ya Polisi Dodoma, hivyo Polisi Mkoa wa Kinondoni ‘mikono yao imefungwa’.

“Tumeomba dhamana kwa bahati mbaya RCO Msangi (Davis Msangi)amesema yeye mikono yake imefungwa kwa sababu mlalamikaji ni makao makuu ya Polisi Dodoma, kwa mujibu wa sheria Polisi wanatakiwa kumshikilia sio zaidi ya saa 24.

“Kwa kuwa alikamatwa saa kumi tarehe 18 tunatarajia mpaka leo hii saa 10 jioni saa 24 zitakuwa zimeshatimia, baada ya hapo tutachukua hatua za kisheria kuhakikisha Polisi wanalazimishwa kwa mujibu wa sheria kumpa dhamana,”alisema na kuongeza Mwasipu.

Chanzo: Mwananchi