Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Waziri Mbarawa atishia kuzifutia usajili kampuni nne za ujenzi

Video Archive
Sat, 21 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Waziri wa Maji nchini Tanzania, Profesa Makame Mbarawa ametishia kuzifutia usajili kampuni nne za ujenzi wa miradi ya maji nchini ikiwemo ya

Mbesso Construction Limited inayojenga mradi wa maji kijiji cha Tela Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Desemba 21, 2019 alipotembelea mradi huo na kubaini utekelezaji wake kusuasua na kuwepo wa udanganyifu, “wameweka gharama kubwa. Mbesso ni mkandarasi ambaye tuna shida naye.”

“Kuna miradi kama saba au nane anayoitekeleza na gharama yake ni ya ajabu. Niliona mlivyokuwa Mwakalidi Mbeya kibanda tu mmetenga Sh100 milioni na hiki kibanda hapa Moshi nimeona mmetenga Sh55 milioni ndio

maana nimeshtuka nikaja nione.”

miradi yenu bei nazo zipo juu, nimepitia miradi yenu yote

na bei zote ziko juu, sasa tutaupitia mradi wote huu, mimi siamini

kama mradi huu gharama yake ni Sh900 milioni,” amesema Mbarawa.

Ameongeza, “nataka watu waje  wapitie upya mradi huu tujiridhishe. Tukiridhika haki yako utaipata. Serikali hatupendi mtufanyie ujanja, nataka nimuandikie

msajili wa makandarasi tukufutie usajili wako.”

Amesema kampuni hiyo inafanya mawasiliano na maofisa wa Wizara ya Maji kuidanganya Serikali, wamekuwa wakikwamisha miradi mbalimbali.

 “Sitatoa vibali kwa sababu nawachukia makandarasi waongo, sio

waadilifu na mnadanganya mnaweka bei za juu, kuna wahandisi wawili

watakuja kukagua mradi huu hatuwezi kwenda namna hii,” amesema Mbarawa.

Msimamizi wa mradi huo aliyejitambulisha kwa jina moja la Benjamin alipoulizwa kuhusu gharama za ujenzi amesema zipo juu kutokana na mazingira na umbali.

Chanzo: mwananchi.co.tz