Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Unicef yataja mambo matano yanayohusu ukuaji wa mtoto

Video Archive
Wed, 18 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mtaalamu kutoka Idara ya Maendeleo ya Awali ya Mtoto kutoka Shirika la kuhudumia watoto Dunia (Unicef), Tuzie Edwin ametaja mambo matano muhimu yanayohusu ukuaji wa mtoto.

Amesema ili mtoto akue vizuri na kufikia ndoto zake za kimaisha anahitaji lishe bora, uhakika wa huduma za afya, usalama, ulinzi na uchangamshi kwa maana ya michezo na mawasiliano.

Tuzie alizungumza hayo jana Jumatatu Desemba 16, 2019 jijini Dar es Salaam katika kongamano kuhusu Haki za Mtoto lililoandaliwa kwa pamoja baina ya Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (Unicef), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Alisema kwa sababu asilimia 80 ya ubongo wa binadamu huanza kutengenezwa tangu akiwa tumboni na mara baada ya kuzaliwa katika makuzi yake ya awali kuna kila sababu ya kuhakikisha anaandaliwa vizuri.

Tuzie alisema wataalamu wa uchumi wamekisia kwamba taifa linalowekeza kwenye ukuaji wa awali wa mtoto linaweza kupata faida kubwa hapo baadaye.

“Taifa likiwekeza dola moja kwenye maendeleo ya awali ya mtoto, linaweza kupata faida ya dola 17 mtoto huyo akikua,” alisema Tuzie.

Awali, Mhadhiri wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Abigail Kweli alisema ulinzi wa mtoto huanzia kwenye familia.

Alisema yapo mambo mengi yanafanywa kwenye familia yanayotishia ulinzi wa mtoto ikiwamo matumizi mabaya ya mitandao.

Chanzo: mwananchi.co.tz