Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Unicef inavyotizama changamoto ya watoto Tanzania

Video Archive
Wed, 18 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (Unicef) Rene’van Dongen amesema japo zipo hatua zilizo chukuliwa na Serikali ya Tanzania kuboresha utoaji wa huduma kwa watoto, kuna changamoto zinazohitaji mikakati ya kuzimaliza.

Ametaja changamoto inayohitaji jitihada za kuimaliza ni vifo vya watoto wachanga kabla na baada ya kuzaliwa ambapo takwimu zinaonyesha kila mwaka watoto 38,000 wanafariki dunia.

Tanzania ni kati ya nchi zinazoadhimisha miaka 30 ya Mkataba wa Haki za Watoto (CRC)  huku ikifanikiwa kutunga Sheria ya Mtoto ya mwaka 2019.

Dongen alisema hayo jana Jumatatu, Disemba 16, 2019 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza kwenye Kongamano kuhusu Haki za Mtoto lililoandaliwa kwa pamoja baina ya Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (Unicef), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Kuhusu mafanikio, Dongen amesema Tanzania imefanikiwa kuongeza idadi ya watoto shuleni na kuboresha huduma za afya hasa kwa mama na mtoto.

Hata hivyo, alitaja changamoto zinazoendelea kukabili utoaji wa huduma hizo kwa mtoto ni pamoja na vifo vya watoto kabla na baada ya kuzaliwa.

Mwakilishi huyo mkazi wa Unicef alisema Takwimu zinaonyesha Tanzania ni kati ya nchi zenye idadi kubwa ya watoto wanaokufa kabla na baada ya kuzaliwa.

“Watoto 38,000 wanakufa kila mwaka na asilimia 78 kati yao wanakufa baada tu ya kuzaliwa, tunawezaje kumaliza vifo hivi? Hili la kufanyia kazi,” alisema Dongen.

Kuhusu changamoto ya ndoa, alisema msichana mmoja kati ya watatu chini ya umri wa miaka 18 anaingia kwenye ndoa za utotoni na kukatisha ndoto zake kielimu.

Hata hivyo, alisema zipo changamoto zinazotakiwa kuendelea kufanyiwa kazi ikiwamo vifo kabla na baada ya kuzaliwa,

Naibu Waziri wa afya nchini Tanzania, Dk Faustine Ndungulile alikiri kuwapo kwa changamoto kadhaa zinazokabili kundi la watoto na kwamba, ipo mikakati inayofanywa kukabiliana nayo.

Chanzo: mwananchi.co.tz