Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Shughuli Dar es Salaam zinaendelea kama kawaida

Video Archive
Thu, 20 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar  es Salaam. Licha yakuwapo kwa tishio la ugaidi lililotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, baadhi ya wakazi wa eneo la Masaki, Dar es Salaam wamesema hawana taarifa.

Jana Jumatano Juni 19, 2019 Ubalozi huo ulieleza kuwapo kwa uvumi wa kutokea kwa shambulio la kigaidi katika eneo la Masaki hususan hoteli za kitalii na maduka ya maeneo hayo ya ufukwe wa Bahari ya Hindi.

Ubalozi huo uliwataka wakazi kuwa makini na maeneo hayo, kujiepusha na makundi na kufuatilia taarifa kupitia vyombo vya habari.

Leo Alhamisi Juni 20, 2019 Mwananchi limezungukia maeneo kadhaa yaliyoelezwa  huenda kukatokea kwa shambulio na kushuhudia wananchi wakiendelea na shughuli kama kawaida.

Akizungumza na Mwananchi, Kamishna wa Ushirikishwaji Jamaii wa Jeshi la Polisi, Musa Ali Musa alisema licha ya hali kuwa shwari makosa yamepungua kutokana na takwimu.

"Haya matishio tumeyasikia kupitia kwenye vyombo vya habari, nchi iko shwari kwetu sisi ni kazi ya kila siku na jeshi la polisi limejipanga," alisema Mussa

Pia Soma

Alisema wanawashirikisha wenye mahoteli na wananchi na kama yapo wataendelea kuyafanyia kazi kuhakikisha nchi inabaki salama.

Baadhi ya wananchi  waliozungumza na Mwananchi katika maeneo ya Masaki jijini humo wanasema wameshangazwa na taarifa hizo.

Dereva wa bajaji anayeegesha nje ya moja ya hoteli za maeneo ya Masaki, Shabani Suleman amesema hana taarifa kuhusiana na tishio hilo.

"Mimi kijiwe changu kila siku ni hapa hakuna mtu yoyote aliyetuletea taarifa hata kwenye vyombo vya habari sijaona " amesema Shabani.

Mfanyabiashara Shomari Shomari amesema hana taarifa yoyote kuhusiana na kuwapo kwa tishio hilo ndiyo kwanza amesikia leo baada ya kuona waandishi wa habari.

"Mimi huwa nafungua hapa saa moja kasoro wakatia napanga vitu vyangu ndio wamepita waandishi wakaanza kunihoji," amesema Shomari

Chanzo: mwananchi.co.tz