Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Profesa Lipumba adai demokrasia inaminywa Tanzania

Video Archive
Wed, 2 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora . Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba amesema mkakati wa kuminya  demokrasia unaofanywa na chama tawala na vyombo vya dola ni mkakati wakutaka upinzani kukata tamaa .

Ameyasema hayo leo Oktoba 2,2019 wakati akiongea na viongozi wa wilaya, na wanachama wanaotegemea kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa vijiji, vitongoji na mitaa.

Amesema ni muhimu kila mmoja kufahamu kanuni za uchaguzi kwa kuwa mkakati uliopo ni wagombea kupita bila kupingwa

Mwenyekiti huyo wa Chama cha wananchi CUF amesema ukosefu wa haki umekithiri hadi kwenye taaarifa ya umoja wa mataifa kuhusu hali ya furaha kwa wananchi.

"Tunahitaji mabadiliko kuelekea 2020  ili tuwe nchi ambayo watu wale hawakati tamaa na inakuwa nchi yenye furaha" amesema

Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano ya Umma wa CUF Abdul Kambaya amesema kufanya maamuzi sahihi kwa watu au vitu inahitaji kujitambua.

Pia Soma

Advertisement
Amesema mkoa wa Tabora  umepata bahati ikiwemo kuwa waasisi na wazee waliotumika kupigania uhuru.

"Mkoa wenu umepewa bahati ya wazee wenu kupigania uhuru lakini mmepewa mtu anayeheshimika Duniani" amesema Kambaya

Profesa Lipumba anafanya ziara hiyo kuhamasisha uchaguzi wa Serikali za mitaa na uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Chanzo: mwananchi.co.tz