Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Ofisi ya msajili yabariki Fahmi Dovutwa kuvuliwa Uenyekiti wa UPDP

Video Archive
Tue, 14 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania, imebariki kuvuliwa uenyekiti kwa Fahmi Dovutwa wa Chama cha United Peoples Democratic Party (UPDP).

Wakati msajili akibariki hilo,wanachama wa chama hicho wamesema bado wanamtambua Dovutwa kama Mwenyekiti wao kwa kuwa kikao kilichomvua madaraka sio halali na kueleza kuwasajili anatumika kuwavuruga.

Katika tamko lao lililosomwa  leo  Jumatatu Januari 13,2020,mbele ya waandishi wa habari na mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa,Asha Chuma, wanachama hao wamesema bado wanamtambua kiongozi huyo kwa kuwa kwa mujibu wa katiba ya UPDP ibara 15(3)(d) mamlaka ya nidhamu ya Mwenyekiti wa Taifa ni mkutano mkuu na sio vinginevyo.

"Kwa mujibu wa katiba yetu Mkutano mkuu ndio unaomchagua Mwenyekiti lakini pia unaweza kumuondoa ikiwa kuna sababu za msingi za kufanya hivyo na si vinginevyo hivyo kitendo cha msajili kubariki kikao cha Halmashari kumng'oa Mwenyekiti hakikubaliki na aelewe bado tunamtambua Dovutwa kama Mwenyekiti wetu," Amesema Asha.

Mwananchi ilimtafuta Msajili Msaidizi wa vyama vya siasa nchini, Sisty Nyahonza, Sisty Nyahonza, ambaye amekiri kupokea taarifa ya kikao cha Halmashauri Kuu Taifa kupitia Katibu Mkuu wa UPDP, ya kumvua madaraka Dovutwa.

Nyahoza amesema baada ya kupitia nyaraka hizo amejiridhisha kuwa kikao hicho na maamuzi iliyoyafanya yalikuwa halali kwa mujibu wa katiba na kanuni za chama hicho.

Hata hivyo msajili huyo amesema kama Dovutwa hajaridhika na maamuzi hayo anatakiwa akate rufaa na sio kulalamika kutumia vyombo vya habari.

Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam,Nassori Lugome,amesema kutokana na sintofahamu hiyo ,Mwenyekiti na Katibu mkuu wanapaswa kuitisha mkutano mkuu wa dharura mara moja.

"Japokuwa mkutano mkuu ulipaswa kufanyika Desemba mwaka jana ukashindikana kutokana na mgogoro huu,ukasogezwa hadi Aprili,2020 lakini kwa hiki kinachoendelea Mwenyekiti na Katibu waitishe mkutano huo mara moja ndani ya miezi hii miwili.

" Pia  na tuhuma zinazoelekezwa dhidi ya Mwenyekiti zipelekwe katuka mkutano huo  ili wanachama waamue mini cha kufanga  kwa kufuata katiba na sheria ya chama,"

amesema Lugome.

Chanzo: mwananchi.co.tz