Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Msukuma kuwasilisha hoja binafsi bungeni, Waziri Biteko amjibu

Video Archive
Thu, 17 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Geita. Mbunge wa Geita (CCM) nchini Tanzania, Joseph Kasheku ‘Musukuma’ amesema atapeleka hoja binafsi bungeni kupinga uamuzi wa Serikali wa kuzuia matumizi ya Zebaki.

Septemba 10, 2019 Bunge la Tanzania liliridhia mkataba wa Minamata kuhusu Zebaki unaolenga kupiga marufuku matumizi ya zebaki katika shughuli mbalimbali baada ya kubainika una athari kwa mazingira na viumbe hai hususan kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu.

Akizungumza leo Jumatano Oktoba 16 ,2019 katika kikao cha ushauri cha mkoa wa Geita, Msukuma amesema anapinga uamuzi wa kuzuia kwa zebaki kwakuwa amekulia kwenye maeneo yanayotumia zebaki na hajaona madhara yanayosababishwa na Zebaki.

Msukuma amesema  uchunguzi zaidi wa madhara ya Zebaki unapaswa kufanywa kwakua mkataba wa Menamata ulisainiwa toka mwaka 2006 na hakukuwa na kuwatisha wachimbaji  kama ilivyo sasa ambapo imetokea baada ya Serikali kubana na kuanzisha masoko ya dhahabu ili kuongeza mapato.

Msukuma amesema badala ya kuzuia matumizi ya Zebaki ni vema Serikali ikaweka nguvu kwenye wizara ya afya na kupambana na magonjwa ya saratani, kisukari na Ukimwi badala ya kuwatoa wachimbaji kwenye teknolojia waliyozoea na kusababisha uzalishaji wa dhahabu kushuka.

Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumzia suala hilo amesema wabunge waliridhia mkataba wa Menamata akiwemo Msukuma bungeni na kwamba kwakuwa atapeleka hoja binafsi  haingilii hoja yake lakini anaamini atapata majibu sahihi pindi akiipeleka.

Pia Soma

Advertisement
Biteko amesema tafiti mbalimbali zimefanyika na zimeonyesha madhara ya Zebaki  na kusema hata uchenjuaji wa dhahabu hautoi dhahabu kwa asilimia zote na kwamba ni asilimia 30 tu ya dhahabu hutolewa huku asilimia 70 zikipotea.

Akizungumza bungeni wakati wa kuwasilisha azimio la Bunge la kuridhia mkataba wa Menamata  kuhusu Zebaki, Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene alisema inakadiriwa asilimia 25 hadi 33 ya wachimbaji wadogo wa dhahabu hapa nchini wameathiriwa na Zebaki.

Alitaja baadhi ya madhara yaliyosababishwa na Zebaki ni wachimbaji kupata magonjwa yakiwemo yale ya mifumo ya neva za fahamu, uzazi, upumuaji, figo, moyo na udhaifu wa mwili.

Mkataba wa menamata ulianza kutekelezwa Agosti 16, 2017 baada ya nchi 50 kuridhia kama inavyotakiwa na Ibara ya 30 na mkataba huo ambapo Serikali ya Tanzania imelenga kupunguza matumizi ya Zebaki kwa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kwa asilimia 30 ifikapo mwaka 2024.

 

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz