Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Msaidizi wa Nyerere afichua maagizo mawili aliyopewa London

Video Archive
Tue, 8 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Msaidizi wa Mwalimu Julius Nyerere ameeleza namna alivyopewa maagizo mawili muhimu na Baba huyo wa Taifa kabla ya kukutwa na umauti.

Oktoba 14, 2019 Mwalimu atatimiza miaka 20 tangu afariki dunia akiwa kwenye Hospitali ya Mtakatifu Thomas jijini London, Uingereza alikokwenda kwa matibabu.

Balozi Charles Sanga, ambaye ni mmoja wa wasaidizi wa Rais huyo wa Kwanza wa Tanzania, anaelezea hali ya Mwalimu ilivyokuwa wakati wakiondoka nchini kwenda London kwa ajili ya matibabu na namna alivyokuwa huko kabla ya kulazwa katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas.

Balozi Sanga alifanya mahojiano maalumu na Mwananchi kuhusu miaka 20 baada ya kifo cha Mwalimu Nyerere.

Balozi Sanga anasema Mwalimu kabla hajafariki dunia, yeye alipata bahati ya kuwa msaidizi pekee aliyezungumza naye kwa takriban saa moja jijini London.

“Septemba 22, 1999 Mwalimu alisema anapenda kwanza aongee na daktari wake, halafu walinzi wake na mwisho alitaka niende mimi pekee yangu,” anasema Balozi Sanga.

Pia Soma

Advertisement
Anasema alienda kwa Mwalimu akiwa na mafaili yaliyokuwa na nyaraka mbalimbali akijua ni mazungumzo ya kikazi, lakini alipofika aliambiwa ayaweke pembeni avute kiti akae jirani naye.

“Charles nakufa, hivyo mtanizika na fikra zangu, mtanizika na nia zangu kwa ajili ya nchi yangu, matamanio yangu kwa ajili ya nchi yangu, mtazika vyote hivyo? Mwalimu alimwambia Balozi Sanga kwa njia ya swali.

Kwa habari zaidi soma gazeti la Mwananchi la leo Jumanne Oktoba 8, 2019.

Chanzo: mwananchi.co.tz