Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Mrema: Mimi ni nani hata nimkatalie Rais

Video Archive
Wed, 17 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Parole, Augustino Mrema jana amemaliza muda wake kuongoza bodi hiyo na kubainisha changamoto saba zinazotakiwa kufanyiwa kazi ili chombo hicho kitekeleze majukumu yake kwa ufanisi.

Aidha, amesema iwapo Rais ataona anafaa kuendelea kwa miaka mingine mitatu yupo tayari.

Parole ni utaratibu wa kisheria unaomwezesha mfungwa anayetumikia kifungo kirefu kuachiliwa kwa masharti maalumu kabla ya kifungo chake kumalizika na kwenda kutumikia sehemu ya kifungo kilichobakia kwenye jamii.

Mrema alieleza jana wakati wa mkutano na wanahabari uliofanyika nyumbani kwake, Salasala uliolenga kutoa shukrani kwa Rais John Magufuli na uongozi wa magereza kisha kueleza utendaji wa bodi hiyo katika kipindi cha Julai 16, 2016 hadi Julai 16 mwaka huu.

Alisema changamoto alizozibaini ndani ya bodi hiyo ni kuchelewa kuteuliwa wajumbe wawili mara baada ya mwenyekiti wa Parole kuteuliwa, Waziri wa Mambo ya Ndani kuchelewesha kusaini mafaili anayopelekewa ili kuruhusu wafungwa kuachiliwa.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz