Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Miss Tanzania 2019 kuzawadiwa Sh10 milioni

Video Archive
Tue, 20 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kamati ya Miss Tanzania imesema mlimbwende atakayevikwa taji la mwaka 2019 atazawadia Sh10 milioni.

Warembo 20 kutoka Kanda saba watachuana Ijumaa ijayo katika ukumbi wa Millenium Tower Kijitonyama jijini Dar es Salaam kusaka mshindi wa mwaka 2019.

Mkurugenzi wa kampuni ya The Look, Basila Mwanukuzi amesema wameamua kutoa zawadi ya fedha ili mrembo atakayeibuka mshindi aamue nini atazifanyia fedha hizo.

Basila aliyewahi kuwa Miss Tanzania 1998,  amesema mbali na fedha hiyo, mshindi ataiwakilisha nchi kwenye mashindano ya dunia.

Alisema kamati yao imelipia Sh20 milioni kwa ajili ya mshiriki wa Tanzania kwenye shindano hilo la ngazi ya dunia.

"Maandalizi yamekamilika na tayari tumepata washindi  wa mataji madogo  ambao watatangazwa siku ya fainali,” amesema Basila.

Pia Soma

 

Chanzo: mwananchi.co.tz