Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Miili waliokufa kongamano la Mtume Mwamposa yawasili uwanja wa mashujaa

Video Archive
Mon, 3 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi.  Vilio na simanzi vimetawala katika viwanja vya Mashujaa mjini Moshi mkoani Kilimanjaro baada ya kuwasili miili ya watu 20 waliokufa Jumamosi Februari Mosi, 2020 katika kongamano wa Nabii na Mtume, Boniface Mwamposa (Buldoza).

Mwamposa anadaiwa kuendesha ibada na kuwaelekeza waumini wake kukanyaga mafuta yaliyokuwa yamemwagwa juu ya kasha ambalo ndani  yake lilitandikwa plastiki zito lililomwagiwa mafuta, jambo ambalo inadaiwa lilichangia vifo vya watu 20 na wengine 16 kujeruhiwa kutokana na kukanyagana.

Ibada ya kuaga miili hiyo inafanyika leo Jumatatu Februari 3, 2020 katika viwanja hivyo. Ibada hiyo imehudhuria na viongozi mbalimbali huku idadi ya wananchi ikiwa kubwa.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Chanzo: mwananchi.co.tz