Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Mbunge wa Rufiji afikisha kilio cha mafuriko bungeni

Video Archive
Wed, 1 Apr 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Rufiji nchini Tanzania (CCM),  Mohamed Mchengerwa amehoji hatua zinazochukuliwa na Bunge kuwaangalia watu waliokumbwa na maafa ya mafuriko kwenye wilaya hiyo ambao ni kati ya 20,000 hadi 50,000.

Mchengerwa amewasilisha kilio hicho leo Jumanne Machi 31 2020 mara baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kutoa taarifa ya utaratibu waliouweka katika kujikinga na virusi vya corona.

Mbunge huyo amesema nchi yote imekumbwa na mafuriko yaliyosababisha maumivu kwa wanyama, binadamu na miundombinu na vitu vingine vingi.

Hata hivyo, amesema pamoja na kwamba mafuriko yamejitokeza kwenye maeneo mbalimbali nchini lakini yapo yamesababisha maumivu makubwa ikiwemo Rufiji.

“Wananchi zaidi ya 20,000 hadi 50,000 wamekuwa hawana maeneo ya kuishi, vyakula na wamekuwa wakipambana kuokoa maisha yao. Je kama Bunge tunachukua hatua gani kuwaangalia wananchi hao wanyonge ambao pia wako katika maafa ya mafuriko? Amehoji. Akijibu Spika Ndugai amesema Serikali imepata ujumbe huo na imeendelea kuchukua hatua.

Hata hivyo, amesema  wakati fulani wataiomba Serikali iwape taarifa kuhusu mambo yanayoendelea wilayani humo na hivyo kujua nafasi ya Watanzania wote kuwasaidia

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz