Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewatia hatiani washtakiwa watatu akiwemo raia wa China, Yang Feng Glan (66) waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka ya kufanya biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh 13bilioni.
Mbali na Glan, maarufu kama Malkia wa Tembo, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Salvius Matembo na Philemon Manase.
Akizungumza leo Jumanne Februari 19, 2019, hakimu mkazi mkuu wa mahakama hiyo, Huruma Shaidi amesema amewatia hatiani washtakiwa hao.
Hata hivyo, mahakama hiyo, itatoa adhabu leo saa tano asubuhi hii na kesi imeahirishwa kwa muda.
VIDEO: Hukumu kesi ya Malkia wa Tembo Februari 19