Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Mahakama kutoa uamuzi Erick Kabendera kumuaga mama yake

Video Archive
Thu, 2 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam nchini Tanzania  imepanga saa 8:45 mchana wa leo Alhamisi Januari 2, 2020 kutoa  uamuzi wa kumruhusu mwandishi wa habari nchini humo, Erick Kabendera kwenda au kutokwenda kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa mama yake mzazi Verdiana Mujwahuzi (80).

Uamuzi huo unatarajia kutolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Janeth Mtega baada ya wakili wa mshtakiwa, Jebra Kambole kuwasilisha mahakamani hapo ombi la kuiomba mahakama hiyo imruhusu mteja wake kwenda kutoa heshima za mwisho kwa mama yake mzazi, akiwa chini ya ulinzi.

Verdiana aliyefariki dunia Desemba 31, 2019 katika Hospitali ya Rufaa Amana jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa siku mbili kwa ajili ya matibabu.

Kesho Ijumaa mwili wa Verdiana utaagwa kisha kusafirishwa Jumamosi Januari 4, 2020 kwenda Bukoba kwa mazishi.3

>Erick amefikishwa mahakamani hapo akitokea Gereza la Segerea Dar es Salaam kusikiliza kesi inayomkabili ya utakatishaji fedha ambapo mashtaka yanayomkabili hayana dhamana.

Mashtaka yanayomkabili ni kupanga na kushiriki mtandao wa uhalifu, kukwepa kodi zaidi ya Sh173 milioni na utakatishaji fedha zaidi ya Sh173 milioni.

Erick alipandishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Agosti 5, 2019 ikiwa ni siku ya saba tangu alipokamatwa na Polisi Julai 29, 2019 akiwa nyumbani kwake Mbweni, Dar es Salaam.

Chanzo: mwananchi.co.tz