Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: DPP kumchukulia hatua Lema, adai ametoa taarifa za uongo

Video Archive
Fri, 13 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga amesema watamchukulia hatua Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kwa kitendo chake cha kusambaza taarifa za uongo kuhusu mauaji ya watu 14 wilayani Manyoni mkoani Singida.

Lema anadaiwa kutoa taarifa hizo hilo Februari 2020 wakati akizungumza katika mazishi ya katibu wa Chadema jimbo la Singida Mashariki, Alex Joas ambaye mwili wake ulikutwa kando ya barabara ukiwa na majeraha kichwani.

Machi 2, 2020 mbunge huyo ambaye pia mjumbe wa kamati kuu Chadema alikamatwa na polisi jijini Arusha na kusafirishwa usiku hadi Singida kwa hatua zaidi, baadaye aliachiwa kwa dhamana

Leo Alhamisi Machi 12, 2020  Mganga amewaambia wanahabari kuwa watamchukulia hatua mbunge huyo ingawa hakuweka wazi hatua gani, akisisitiza anazifahamu yeye mwenyewe.

‘Hatua nitakazozichukua nazifahamu mimi na ofisi, mtaziona wakati nitakapozichukua kwa sababu hazitafanyika kwa kificho kama nitamshtaki au la nitaangalia," amesema Mganga.

Katika maelezo yake, Mganga amesema taarifa zilizotolewa za mbunge huyo si kweli akisema amepitia jalada moja baada ya nyingine na kubaini polisi wamezifanyia kazi taarifa hizo tofauti na maelezo ya Lema.

Pia Soma

Advertisement

"Hata kama sifa za kisiasa basi tuwe na mipaka, kuna marehemu mwingine kifo chake kimesababishwa na ajali ya pikipiki lakini mheshimiwa Lema katika taarifa yake amesema amechinjwa. Mwingine alishambuliwa na fimbo, mateke na ngumi lakini anataja wamechinjwa huu ni uongo," amesema Mganga.

Mganga amehoji kama watu hao wamechinjwa kwa nini Lema hakuenda kutoa taarifa polisi, hadi anafikia hatua ya kusema polisi wameshindwa kuwakamata watuhumiwa waliotekeleza mpango huo.

"Tunapochukua hatua nitaomba mnielewe, hatuwezi kuendelea kuwa na Taifa lenye watu wenye uzushi na kueneza taarifa zenye taharuki zinazosababisha chuki kwa Watanzania. Narudia sitajali mwanasiasa wa chama chochote, rangi, kabila wala cheo yeyote anayefanya makosa nitamfungulia mashtaka.”

"Kwa hili lazima nitachukua hatua hatuwezi kuendelea na upotoshaji na uvunjifu wa namna hii. Halafu watu wanatoka na kusema wanasiasa wa upinzani wanaonewa wakati wanafanya upuuzi wa namna hii, haiwezekani, tusijifiche kwenye siasa kwa ajili ya kuvuruga  amani, "amesema  Mganga.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz