Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Bosi Jeshi la Zimamoto na uokoaji alilia uhaba wa watumishi

Video Archive
Wed, 18 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Tanzania, Thobias Andengenye amesema jeshi hilo lina uhaba wa zaidi ya watumishi 4,000 nchini.

Kamishna Andengenye ameyasema hayo leo Jumatano Desemba 18, 2019 katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa jengo la Zimamoto na Uokoaji la Wilaya ya Chato mkoani Geita na uzinduzi wa Mahakama ya Chato.

Amesema ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi jeshi hilo linahitaji kuwa na rasilimali inayotosheleza lakini kwa sasa jeshi hilo linakabiliwa na uhaba mkubwa wa watumishi.

“Rais ili kutekeleza majukumu kwa ufanisi kuendana na vituo na vifaa vilivyopo, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linahitaji kuwa na watumishi 7,076 ili kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwenye vituo vilivyopo lakini kwa sasa watumishi waliopo kwenye vituo ni 2,154 kwa nchi nzima,” amesema

Amesema katika kusogeza huduma za Zimamoto na Uokoaji karibu na wananchi jeshi hilo lina jumla ya vituo 93 vya Zimamoto na Uokoaji nchi nzima lakini bado watumishi wa kujaza vituo hivyo bado ni changamoto.

“Jeshi limefanikiwa kuanzisha vituo katika mikoa yote Tanzania Bara, jeshi hilo lina jumla ya vituo 93 vya Zimamoto na Uokoaji na jitihada zinaendelea kusogeza vituo katika wilaya”

kizungumzia gharama za ujenzi wa jengo hilo la Zimamoto la Wilaya ya Chato amesema limegharimu Sh713.6 milioni kwaajili ya ujenzi wa ofisi na kituo cha wilayani Chato na ujenzi huo ulianza Oktoba 2019 na unakamilika Februari 2020.

 “Rais naomba upokee shukrani zangu kwa kulipatia Jeshi la Zimamoto na uokoaji Sh713.6 milioni kwa ajili ya ujenzi wa ofisi na kituo cha jeshi la Zimamoto na uokoaji hapa wilayani Chato ambacho kitaimarisha shughuli za uokoaji wa maisha na mali za wananchi wilayani Chato,” amesema

Amesema jengo hilo likikamilika litakuwa limegharimu zaidi ya Sh900 milioni ikiwa ni gharama za ujenzi pamoja na thamani za ndani

“Thamani za ndani zitagharimu Sh229 milioni hivyo kufanya jumla ya gharama za ujenzi wa jengo hilo na thamani kufikia hadi kukamilika kwake Sh943 milioni” amesema

Chanzo: mwananchi.co.tz