Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Askofu Shao aeleza madhara ya uhujumu uchumi

Video Archive
Thu, 24 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar, Augustino Shao amesema kinachoendelea hivi sasa nchini Tanzania kuhusu tuhuma za uhujumu uchumi kwa watu mbalimbali ni matokeo ya kujilimbikizia mali, kutotumia utajiri wao kuwasaidia wengine.

Amesema ubinafsi wa kutaka mali kumnufaisha mtu mmoja au familia yake ni kikwazo kikubwa katika uchumi hasa wa Taifa linaloendelea kujijenga.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Oktoba 24, 2019 wakati akifungua warsha ya siku mbili inayohusu masuala ya uchumi kwa vijana.

Askofu Shao amesema jambo hilo linapaswa kutafutiwa ufumbuzi, kubainisha kuwa hatua inayochukuliwa sasa na serikali imedhihirisha ni kiasi gani matajiri wanashindwa kutumia fedha zao kusaidia wengine na Taifa.

“Sasa hivi wahujumu uchumi wanakiri na kuomba msamaha na ama haitoshi wanarudisha fedha, hebu tujiulize fedha zile zote zilikuwa wapi.”

“Unawezaje kurundika benki kiasi kikubwa vile cha fedha wakati ungeweza kuzizungusha kwenye uchumi, ukatengeneza ajira na kuokoa maisha ya watu,” amesema.

Pia Soma

Advertisement
Ameongeza, “sasa wanalazimishwa kuzirudisha na zitatumika kwenye ujenzi wa miradi mikubwa, nawasihi vijana wasiige mfumo huu wafanye kazi na wakipata fedha wawe tayari kusaidia wengine.”

Chanzo: mwananchi.co.tz