Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Askofu Ruwa'ichi awataka Watanzania kujitathimini, kubebana katika maisha

Video Archive
Fri, 27 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Askofu Mkuu Mwandamizi Jude Thadeus Ruwa'ichi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar Es Salaam nchini Tanzania ameshauri kila Mtanzania na Taifa kwa ujumla kujitathmini maisha aliyoyaishi mwaka 2019 kabla ya kuingia mwaka mpya 2020.

Askofu Ruwa'ichi ametoa kauli hiyo alipoulizwa na Mwananchi ni mambo gani angetamani kuona yakikomeshwa katika jamii kwa sasa.

Ilikuwa ni dakika chache baada ya kumaliza misa ya mkesha iliyofanyika usiku wa kuamkia leo Jumatano Desemba 25,2019 katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jijini Dar es Salaam.

Misa hiyo maalumu ilifanyika ikiwa ni sehemu kusherehekea sikukuu ya Krisimasi, inayoadhimishwa kila mwaka na Wakristo duniani kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu Kristo ili kuukomboa ulimwengu.

"Tunapoelekea kuhitimisha mwaka huu na kuanza mwaka ujao 2020, itakuwa ni fursa ya kijitathmini tulivyoenenda 2019 na kujitahidi kupambanua malengo, mipango na vipaumbele vyetu ili tupige hatua katika maisha yetu," amesema Askofu Rweichi.

"Niwaalike Watanzania na waamini wote kuzingatia hitaji la umoja, mshikamano, bidii na uwajibikaji katika majukumu ya kila siku, pia ni muhimu kujiwekea malengo yaliyo mema."

Katika ufafanuzi wake, Askofu Ruwa'ichi amesema Yesu alimpenda mwanadamu hivyo sikukuu ya Krisimasi inawakumbusha Watanzania kudumisha upendo na kutendeana haki na matendo ya huruma.

"Tutambuane na kubebana katika safari ya maisha yetu," amesema

Chanzo: mwananchi.co.tz