Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetemeko: Taarifa za Christian Atsu kupatikana akiwa hai zaichanganya Ghana

Atsu Christian .jpeg Christian Atsu

Thu, 9 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya taarifa kutolewa kuwa mwanasoka wa Ghana, Christian Atsu ameokolewa kutoka kwenye kifusi, Balozi wa Ghana nchini Uturuki, Salamatu Yakubu amekanusha taarifa hizo.

Salamatu sambamba na viongozi wa timu yake wamesema wamemsaka Atsu kila hospitali na kubaini kuwa hakuna iliyompokea wala jina lake halipo kwenye orodha ya manusura mpaka sasa.

Taarifa zinadai kuwa Atsu sambamba na Mkurugenzi wake bado wapo chini ya kifusi na harakati za uokoaji unaendelea.

Awali taarifa kuhusu staa huyo wa zamani wa Chelsea na New Castle United za Uingereza, ambaye kwa sasa anakipiga Hataysport zilidai kuwa amepatikana akiwa hai na anaendelea kupatiwa matibabu hospitalini baada ya kuokolewa kutoka kwenye vifusi kufuatia matetemeko mawili mabaya ya ardhi yaliyokumba Uturuki na Syria.

A Bola inaripoti kuwa Mghana huyo alipatikana hai na kusafirishwa hospitalini baada ya kupata majeraha kwenye mguu wake wa kulia na kushindwa kupumua.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 31, alikuwa amewafungia bao la ushindi waajiri wake wapya Hayatspor katika mechi yao ya Jumapili, Februari 6, muda mfupi tu kabla ya tetemeko la ardhi kutokea nchini humo.

Mwandishi wa habari Saddick Adams pia alithibitisha kwamba amekuwa akiwasiliana na uongozi wa Atsu na kwamba wamethibitisha kuwa winga huyo yuko salama.

Wachezaji wenzake wawili wa Hatayspor pamoja na watalaam wa ushauri pia walisemekana kuokolewa kutoka kwenye vifusi hivyo mapema Jumatatu.

Kufuatia tukio hilo video imeibuka kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha sogora huyo wa zamani wa Newcastle alivyochanja bao hilo huku mashabiki wakisisimka kwa shangwe.

Tetemeko la ardhi Uturuki

Kufikia sasa zaidi ya watu 12,000 wamepoteza maisha nchini Uturuki na Syria baada ya matetemeko hayo na kusababisha uharibifu katika maeneo ya kusini mwa Uturuki na Kaskazini mwa Syria.

Tetemeko la kwanza lilikuwa na ukubwa wa Richter scale 7.8. Idadi ya waliofariki sasa inatarajiwa kuongezeka huku juhudi za kuwaokoa zikiendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: