Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Afrika

Nchi

Kijamii

Sanamu ya Nyerere kujengwa Ethiopia

Pindi Chana Bungeni.jpeg Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Dkt. Pindi Chana

Tue, 6 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Dkt. Pindi Chana leo amewasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka 2023/24 Bungeni Dodoma ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba Serikali inaendelea maandalizi ya ujenzi wa sanamu ya Mwl. Nyerere Makao Makuu ya Umoja wa Afrika Ethiopia ambapo mradi huo utagharimu USD 205,942 (Tsh. Mil 487+).

“Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo inaendelea na uratibu wa maandalizi ya ujenzi wa Sanamu ya Mwl. Nyerere inayotarajiwa kusimikwa Jijini Addis Ababa Ethiopia katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika ambapo hadi Aprili, 2023 hatua iliyofikiwa ni kuanza kwa ujenzi wa Sanamu halisi baada ya Mkandarasi, Kampuni ya EPITOME ARCHITECTS LIMITED ya Tanzania kukamilisha ujenzi wa sampuli kifani ya pili na kuridhiwa na Kamati ya Kitaifa kwa mujibu wa Sheria ya kuwaenzi Waasisi wa Taifa Na. 18 ya mwaka 2004 na Kanuni zake za mwaka 2005.

“Chimbuko la Mradi huo ni mapendekezo ya Hayati Robert Mugabe la mwaka 2015 yaliyolenga kutambua mchango uliotukuka wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika ukombozi wa Bara la Afrika hasa Mataifa yaliyo Kusini mwa Bara hilo”

“Mradi huo wenye thamani ya Dola za Marekani 205,942 unajengwa chini ya usimamizi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Sekretarieti ya SADC, Mameneja Mradi kwa kushirikiana na Familia ya Mwl. Nyerere na kwa mujibu wa mkataba uliopo, inatarajiwa kukamilika Desemba, 2023”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live