Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia: Kuna Mambo Yanashangaza - Video

Video Archive
Wed, 19 May 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Rais Samia: Kuna Mambo Yanashangaza – Video May 18, 2021 by Global Publishers



Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema licha ya kufanyika zoezi la usajili laini za simu kwa kutumia vidole, vitendo vya utapeli na wizi mitandaoni bado vimeendelea kushamiri.

Rais Samia amesema hayo leo Mei 18, 2021 wakati akizindua kiwanda cha ushonaji cha jeshi la polisi kilichopo kilichopo katika Bohari Kuu ya Jeshi la Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam.

“Kuna mambo yanashangaza kulikuwa na sheria wote tusajili laini tuweke vidole ili mtu akifanya utapeli ajulikane lakini utapeli wa mtandao unaendelea na watu hawafikishwi mahakamani, sasa ule usajili ulikuwa kiini macho au nini?

“Maana wote tumesajili na majina yapo. Kwa sababu kama tumesajili vile kila namba inajulikana, na kama kuna zisizojulikana zinatolewa na Shirika gani la simu?” amehoji Rais Samia.

Aidha, Rais amelitaka Jeshi la Polisi kusimamia suala hilo kwa kushirikiana na Taasisi ya Mtandao wa Serikali, TCRA na Taasisi nyingine za fedha za Umma na Binafsi zikiwemo Benki na Kampuni za Simu.

Chanzo: globalpublishers.co.tz