Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Chalamila aeleza sababu ya kutogombea ubunge

Video Archive
Thu, 16 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, ameeleza sababu iliyomfanya kutogombea nafasi ya ubunge kuwa anataka kuhakikisha miradi yote ya Serikali inayotekelezwa katika Mkoa wake anaisimamia vizuri pamoja na kuziratibu shughuli za kimaendeleo.

Chalamila amezungumza hayo leo mbele ya Rais Magufuli katika hafla fupi ya kuwaapisha viongozi wateule Ikulu Chamwino jijini Dodoma, huku akimpongeza Rais kwa kuendelea kukarabati shule kongwe zilizopo mkoani humo.

“Tumepokea Milioni 899 katika Shule ya Sekondari Loleza ambayo mpaka sasa imekwisha kamilika, tumepokea Shilingi Milioni 752 katika Shule ya Sekondari Rungwe ambayo mpaka sasa mchakato wa ukarabati unaendelea, tumepokea Shilingi Milioni 795 kwa Shule ya Sekondari Mbeya Day ambayo nayo mchakato wa ukarabati unaendelea” amesema RC Chalamila.

Aidha Chalamila amempongeza Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguli, kwa kumsaidia kupunguza mihemko kama kijana na kukabiliana na kejeli wa watu zilizotokana na yeye kushikilia misimamo ya sheria.

“Kuna wengine walisema ona kijana huyu anajidai na urefu wake wakijua mimi mfupi, wengine wakasema huyu muhuni anapenda sana mapenzi,lakini tunatukanwa kwasababu tunashikilia sheria” Albert Chalamila-RC Mbeya

Chanzo: www.tanzaniaweb.live