Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PM Majaliwa na Kamati ya Uongozi kuamua hatma ya Polepole, Askofu Gwajima na Jerry Silaa

Video Archive
Fri, 3 Sep 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Hatima ya wabunge watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Askofu Josephat Gwajima (Kawe), Jerry Silaa (Ukonga) na mbunge wa kuteuliwa Humphrey Polepole sasa iko mikononi mwa Waziri Mkuu.

Leo Ijumaa Septemba 3, 2021 wabunge hao waliitwa mbele ya kamati ya Maadili ya wabunge wa CCM na kuhojiwa kutokana na tuhuma zinazowakabili za kusema uongo na kushusha hadhi ya Bunge.

Mwanzoni mwa wiki Bunge lilipokea na kupitisha azimio la Bunge lililowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki,Kinga Madaraka ya Bunge ambalo liliwatia hatiani na kuwapa adhabu ya kutohudhuria vikao vya mikutano miwili ya Bunge Askofu Gwajima na Silaa.

Akizungumza mara baada ya kumaliza kuwahoji wabunge hao, Mwenyekiti wa kamati ya Maadili ya wabunge wa CCM, Hassan Mtenga amesema kazi bado inaendelea.

"Sisi tumemaliza kazi yetu na mapendekezo yanapelekwa kamati ya uongozi ya Bunge ambayo iko chini ya Waziri Mkuu, wakimaliza basi itajulikana nini kinafuata," amesema Mtenga.

Kuhusu Polepole ambaye makosa yake hayakujadiliwa bungeni amesema tatizo lake ni kushabikia mtandaoni mambo yaliyokuwa yakifanywa na Askofu Gwajima.

Soma zaidi:Silaa, Polepole, Gwajima wahojiwa na kamati maadili ya wabunge CCM

Akizungumza kuhusu nini kitatokea kwa wabunge hao ambao tayari walishaadhibiwa kwa kutoshiriki mikutano ya Bunge (Gwajima na Silaa) amesema kamati uongozi itasema mwishoni mwa kazi yao wanayotaraji kuifanya wiki ijayo.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz