Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ole Sabaya Aeleza Ndoa Yake na Jesca Mahakamani

Sabaya Na Mchumba Ole Sabaya Aeleza Ndoa Yake na Jesca Mahakamani

Fri, 4 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya leo Alhamisi, Februari 3, 2022 ameieleza mahakama kuwa amefunga ndoa na Jesca Nassari mwaka 2018 katika kanisa la Arusha Seven Day Adventist.

Sabaya ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kukutwa na hati ya makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha akiwa na wenzake, anaendelea na kesi makosa ya uhujumu uchumi akiwa na wenzake sita na sasa kesi hiyo ipo kwenye hatua ya utetezi baada ya kukutwa na kesi ya kujibu.

Akihojiwa na mawakili wa Jamuhuri, Sabaya amesema amefunga ndoa Mei 27, 2018 na kwamba hakupelekea uthibitisho wowote mahakamani hapo, akisema yeye ndiye huo uthibitisho.

Sehemu ya mahojiano baina ya mawakili wa Jamuhuri na Sabaya

Wakili Neema: Wakati ukitoa ushahidi wako umesema umeoa je umeoa mwaka gani

Sabaya: 2018

Wakili: Nani jina la mke wako.

Sabaya: Jesca Nassari.

Wakili: Mlifunga ndoa lini na wapi.

Sabaya: Ndoa tulifunga kanisa Arusha Seven Day Adventist church 27/5 /2018

Wakili:Wasimamizi wa ndoa walikuwa kina nani.

Sabaya: Elibariki Nnko na Ruth Urassa

Wakili:Unasema ulioa je ulileta uthibitisho wowote mahakamani?

Sabaya: Sijaleta mimi ndio uthibitisho

Wakili: Siku hiyo na tarehe hiyo ulisaini nyaraka kuwa jambo ambalo lilifanya lipo kisheria je ni sahihi.

Sabaya:Ni Sahihi

Wakili: Wakati ukitoa ushahidi ulisema ulikamatwa 27/5/2021

Sabaya: Ni sahihi

Wakili: Wewe ulikuwa miongoni mwa wateule Rais ni sahihi .

Sabaya: Ndio.

Wakili:Uliteuliwa kama mkuu wa wilaya

Sabaya:Ndio.

Wakili:Unakubaliana na mimi kuwa uliapa kiapo.

Sabaya:Ndio niliapa

Wakili:Unakubaliana na mimi kwamba hakuna mtanzania yupo juu ya sheria .

Sabaya:Ndio

Wakili Mtenga:Naomba nianzie kwenye ndoa yako Jesca alisema cheti chake cha ndoa kipo nyumbani.

Sabaya:Jesca alisema ni cha kwake.

Wakili: Wewe cheti chako kipo wapi

Sabaya: Kipo kwangu.

Wakili: Sio nyumba moja na Jesca

Sabaya: Kipo nyumba moja ila kwenye eneo ambalo mimi nimehifadhi.

Wakili: Hujaona umuhimu wa kukileta hapa mahakamani.

Sabaya: Sijaona kwani sina shitaka la ndoa hapa.

Wakili: Uliwahi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM mkoa Arusha.

Sabaya: Ndio

Soma zaidi:Mke wa Sabaya amaliza kutoa ushahidi kesi ikiahirishwa kwa muda

Kesi hiyo itaendelea kesho ambapo Sabaya ataendelea kuhojiwa na mawakili wa Jamuhuri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: