Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nape Ataka Kuundwa kwa Bodi ya Korosho - Video

Video Archive
Mon, 24 May 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

MBUNGE wa Jimbo LA Mtama, Nape Nnauye, amesimamisha bunge kwa dakika kadhaa baada ya kuchangia hoja ya wizara ya Kilimo huku akiwa amejikita katika zao la korosho ambapo amewageuzia kibao Waziri wa Kilimo, Prof. Mkenda, pamoja na Naibu wake, Hussein Bashe.

Nape Nnauye ametaka kuundwa kwa Bodi ya Korosho ambayo haijakuwepo kwa miaka mitatu akihoji, nini lengo la Serikali na zao hilo?

Akiwa Bungeni amesema, “Zao ambalo linaongoza kuingiza Fedha nyingi za kigeni Nchi hii mwaka wa tatu hakuna Bodi. Mkurugenzi yupo anakaimu, na bahati mbaya ninadhani amepewa kazi kubwa kuliko uwezo wake.”

Ameongeza kuwa, Kiongozi huyo ameshindwa kazi na kutaka aletwe mwingine akieleza, “Huyu Mkurugenzi anafika mahali akibanwa na wakulima anaanza kujibu majibu ya kiburi.”

Chanzo: globalpublishers.co.tz