Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naibu waziri awasili eneo la ajali ya treni, atoa neno

Video Archive
Tue, 18 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa amesema hatua ya awali iliyofanywa baada ya kutokea kwa ajali ya lori kugonga treni ya abiri ni kuhakikisha majeruhi katika ajali hiyo iliyotokea jana Jumatatu usiku wanafikishwa haraka hospitali. 

Akizungumza na Mwananchi eneo la tukio karibu na Stesheni ya Dodoma leo Jumanne Juni 18 2019 Kwandikwa amesema amepata taarifa kupitia mtandao na kuamua kufika ili kuona iwapo hatua za wali zimechukuliwa.

“Hatua za awali  kwanza kunusuru abiria waliokuwa kwenye treni kwa kuhakikisha wanakuwa mahali salama. Nashukuru Mungu kwamba majeruhi ambao kwa haraka haraka wamechukuliwa na kupelekwa hospitali (ya Rufaa Dodoma),” amesema.

Amesema shughuli za kunyanyua mabehewa yaliyoanguka zinaendelea na kwamba baadaye wataweza kuangalia namna nzuri zaidi ya kufanya.

Endelea kufuatilia Mwananchi kujua kinachoendelea

Chanzo: mwananchi.co.tz