Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naibu Waziri aagiza Meneja RUWASA kusimamishwa kazi (+video)

Video Archive
Sat, 9 Jan 2021 Chanzo: millardayo.com

Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi Clement Kivegalo kumuondoa Meneja wa Wilaya ya Mbarali (RUWASA), Job Mwakasala pamoja n akufanya mabadiliko ya wataalamu katika wilaya hiyo.

Naibu Waziri amechukua uamuzi huo kufuatia kutoridhishwa na utendaji kazi wao baada ya kukuta changamoto nyingi katika wilaya ya Mbarali huku wakishindwa kuchukua hatua sahihi kuzitatua, ikiwemo kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusiana na utekelezaji na uendeshaji miradi ya maji.

Mhandisi Mahundi amesema wananchi wa wilaya ya Mbarali wana kero nyingi kuhusiana na huduma ya maji huku wasimamizi wakishindwa kuwahudumia badala yake wakitoa taarifa zilizo tofauti ukilinganisha na uhalisia wa hali iliyopo, jambo linalokwamisha jitihada za serikali kutatua kero za wananchi.

Aidha Naibu Waziri huyo ametangaza kuivunja Bodi ya ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Mji Mdogo wa Rujewa katika wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya kwa kushindwa kuisimamia ipasavyo menejimenti ya mamlaka hiyo kutimiza majukumu yake kwa ufanisi kutokana na kubaini ukosefu wa huduma ya uhakika ya maji kwa muda mrefu kwa wakazi wa mji huo bila sababu za msingi.

Chanzo: millardayo.com