Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makada 19 wa CHADEMA wapata dhamana

Chade Ed Makada 19 wa CHADEMA wapatiwa dhamana

Fri, 20 Aug 2021 Chanzo: ippmedia.com

VIONGOZI na wanachama 19 wa Chadema waliofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza leo Agosti 19, wameachiwa huru kwa dhamana baada ya kusomewa shtaka lililokuwa linawakabili.

Akisoma shtaka hilo, Wakili wa Serikali, Bisela Bantulaki ameiambia Mahakama kuwa washtakiwa hao walitenda kosa hilo Agosti 15, 2021 katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kawekamo wilayani Ilemela mkoani humo.

Bantolaki amedai kuwa washtakiwa hao baada ya kufika katika kanisa hilo walianza kufanya fujo wakati ibada ya matoleo ikiendelea.

Akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Emmael Lukumay, Wakili wa upande wa utetezi, Paul Kiheja amedai kuwa kosa walilofanya watuhumiwa hao linadhaminika hivyo anaomba wapatiwe dhamana.

Baada kusikiliza pande zote, Hakimu Lukumay ameagiza watuhumiwa hao kupewa dhamana kwa masharti ya kutoa dhamana ya mali kauli ya Sh1 milioni kila mmoja, kuwasilisha barua ya utambulisho kutoka ofisi ya Serikali ya Mtaa na nakala moja ya kitambulisho cha mpigakura au cha Taifa masharti ambayo waliyatimiza.

"Kwa sababu hakuna pingamizi kutoka upande wa Jamhuri, naagiza washtakiwa hawa wapewe dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana," amesema Bantulaki.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 21 mwaka huu itakapotajwa tena.

Chanzo: ippmedia.com
Related Articles: