Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yaonya upande wa mashtaka kesi ya kutoa lugha chafu dhidi ya Magufuli

Video Archive
Wed, 22 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeonya upande wa mashtaka kuacha kumtegemea shahidi mmoja katika kesi ya kutoa lugha chafu dhidi ya Rais wa Tanzania, John Magufuli inayomkabili mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee.

Imeutaka kuleta mashahidi wote waliobaki ili shauri hilo liweze kuendelea.

Mahakama imeeleza hayo baada ya wakili wa Serikali, Sylivia Mitanto kudai shauri hilo limekuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa lakini shahidi waliokuwa wakimtegemea yupo nje ya Jiji la Dar es Salaam.

“Leo hatuna shahidi tuliyekuwa tukimtegemea yupo nje ya Jiji  la Dar es Salaam hivyo nitajitahidi shauri lijalo kuja na shahidi,” amedai Mitanto.

Baada ya kauli hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema shauri hilo likifika mahakamani upande wa mashtaka umekuwa ukitoa sababu mbalimbali ya kutowaleta mashahidi hao na mara ya mwisho kusikiliza ushahidi ilikuwa Agosti 9, 2018.

“Kwa nini msilete mashahidi wengine kwani huyo ni shahidi wa mwisho, upande wa mashtaka naomba msimtegemee shahidi mmoja nataka siku shauri litakapokuja mje na mashahidi wote ili kesi hiyo iweze kwenda mbele,” amesema Hakimu Simba.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

Waliotoa ushahidi katika si hiyo ni watatu. Shuri hilo limeahirishwa hadi Februari 20, 2020.

Katika kesi ya msingi inadaiwa kuwa Julai 3, 2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema zilizopo mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, Mdee alitamka maneno dhidi ya Rais Magufuli kuwa, “anaongea hovyo, anatakiwa afungwe breki” kitendo kinachodaiwa kuwa ni kumdhalilisha kiongozi mkuu huyo wa nchi na kusababisha uvunjifu wa amani.

Chanzo: mwananchi.co.tz