Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli atuma salamu za rambirambi vifo vya wafanyakazi Azam TV

Video Archive
Mon, 8 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemtumia salamu za pole mwenyekiti wa kampuni za Said Salim Bakhresa kufuatia vifo vya wafanyakazi watano wa vyombo vya habari vya Azam Media Limited waliofariki dunia kwenye ajali ya gari.

Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Julai 8, 2019 eneo la Shelui mkoani Singida  na kusababisha vifo vya wafanyakazi watano wa Azam TV.

Wafanyakazi hao ni kati ya watu saba waliofariki dunia katika ajali hiyo baada ya basi aina ya Coaster walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori wakati wakielekea wilayani Chato mkoani Geita katika uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Chato-Burigi.

“Nimeshtushwa sana na vifo hivi, nampa pole mwenyekiti  Said Salim Bakhresa na ndugu wa marehemu wote,  Mtendaji mkuu Tido Mhando na wafanyakazi wote wa Azam na wanahabari wote ,”amesema Rais Magufuli katika taarifa yake.

Rais Magufuli amewaombea majeruhi watatu wa ajali  hiyo kupona haraka ili kuendelea na majukumu yao ya kila siku, huku akitoa wito kwa watumiaji wa barabara hasa madereva kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Chanzo: mwananchi.co.tz