Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Maajabu ya mapacha walioungana, wanafundisha, kuendesha pamoja (video+)

Video Archive
Wed, 22 Sep 2021 Chanzo: millardayo.com

Leo nakukutanisha na simulizi ya Mapacha wawili walioungana kutoka Marekani, Abigail Hensel (Abby) na Brittany Hensel walizaliwa Marc 07,1990 wakiwa na mwili mmoja lakini kila Mtu ana kichwa chake, moyo wake, tumbo lake , uti wa mgongo na hata mapafu yake.

Abby na Brittany kila mmoja ana mguu mmoja na mkono mmoja ambayo inafanya kazi kwa kushirikiana, kwahiyo hushirikiana kwenye kutembea, kupiga makofi, kuogelea, kukimbia, kuendesha Gari n.k ingawa wana uwezo wa kuongea, kula au kuandika kila Mtu kivyake.

Mapacha hao walizaliwa New Germany , Minnesota Marekani wakasoma hadi Elimu ya Chuo Kikuu, Bethel University na sasa wameajiriwa ni Walimu wanafundisha Sunnyside Elementary , New Brighton.

Chanzo: millardayo.com