Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenyatta amuomba Samia kufuata nyayo za JPM (+video)

Video Archive
Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: millardayo.com

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kufuata nyayo za Hayati Dkt. John Magufuli, kwa kuwa tayari amekwishamuonesha njia ya utendaji kazi na kuwaomba Watanzania kushikamana.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Machi 22, 2021, Jijini Dodoma, kwenye shughuli ya kitaifa ya kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Magufuli, iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

“Na sina shaka nikisema hapa siku ya leo ya kwamba Dada yangu Samia na sasa Rais mwenzangu ya kwamba, barabara umeoneshwa na ndugu yetu Dkt. Magufuli mwito unao, Hapa ni kazi tu, wananchi wa Tanzania wapo nyuma yako endeleeni na umoja mliokuwa nao,” amesema Rais Kenyatta

Awali akizungumza Kenyatta ameeleza ni kwa namna gani Hayati Dkt. Magufuli, alivyokuwa msaada kwa Waafrika, “Kwa muda wa miaka michache ameonesha ya kwamba sisi kama Waafrika tuko na uwezo wa kujitoa kuwa tegemezi kwa watu na nchi za nje na tupo na uwezo kama Waafrika kusimamia uchumi wetu na kuhakikisha ya kwamba wananchi wetu wanatendewa haki”.

Chanzo: millardayo.com