Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ifahamu familia ya Rais Samia, Mama wa kazi kutoka Kizimkazi

Samia 93521 Ifahamu familia ya Rais Samia

Thu, 19 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Samia Suluhu ni Rais wa sita katika Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania.Aliteuliwa kuwa Rais baada ya kifo cha Rais John Pombe Magufuli.Leo tunaangazia familia ya Bi. Samia Suluhu.

Mnamo mwaka wa 1978 Samia Suluhu alifunga ndoa na Bw. Hafidh Ameir. Wakati huo Hafidh Ameir alikuwa afisa wa Kilimo naye Samia alikuwa akifanya kazi kwa Benki moja Zanzibar.

Wanandowa hawa walijaliwa kupata watoto wanne. Mmoja kati ya wanawe, Wanu Hafidh Ameir ni mwakilishi maalum katika Bunge la Zanzibar. Wanawe wengine watatu hawajaingia katika ulingo wa siasa.

Bi Samia Suluhu Hassan aliweka historia kuwa mwanamke wa kwanza kuwa Rais wa Tanzania na pia kuwa makamu wa Rais wa kwanza mwanamke.Samia pia alikuwa Rais wa kwanza katika historia ya Tanzania kuwahi tokea Zanzibar.

Mama Samia Suluhu Hassan kama wanavyomuita kwa mujibu wa tamaduni anatokea kisiwani Zanzibar, ambako watu wengi wanaoishi hapo ni Waisilamu. Bi Suluhu hakuwa maarufu sana katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachotawala.

Kulingana na wachanganuzi wa masuala ya siasa Tanzania, wafuasi wa Magufuli ambao wengi ni wakristo hawakutaka Samia amridhi Magufuli. Hata hivyo, aliungwa mkono na wanachama wa CCM ambao wanamuunga mkono aliyekuwa Rais Jakaya Kiwete, wengi wao wanatoka kwa jamii za Waisilamu. 

Chanzo: www.tanzaniaweb.live