Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Huyu mtoeni" Mkurugenzi aliemdharau Waziri Mkuu atumbuliwa papo hapo (+video)

Video Archive
Sun, 29 Nov 2020 Chanzo: millardayo.com

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza Waendesha Maghala kuacha kukata tozo ya Upungufu wa uzito wa korosho ghafi zilizohifadhiwa ghalani (UNYAUFU) kwa wakulima na wanunuzi kwa kuwa tozo hiyo imeshaondolewa na suala la unyaufu halijathibitishwa kitaalamu.

Ametoa agizo wakati wa kikao kati yake na Wakuu wa Mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara na Ruvuma, Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Kilimo, Viwanda na Biashara pamoja Mrajisi wa Ushirika, Mtendaji Mkuu wa  Bodi ya Korosho, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya  Nafaka na Mazao Mchanganyiko, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Maghala na Waendesha Maghala wote wa Mikoa ya Pwani, Mtwara, Lindi na Ruvuma, kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.

Amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara kumuondoa katika nafasi yake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Maghala Odilo Majengo kwa kushindwa kutekeleza maagizo ya Serikali kuhusu kusitisha tozo ya unyaufu katika zao la korosho.

Chanzo: millardayo.com