Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakuna Kama Eto'o

Etoo Samuel Fillis Hakuna Kama Eto'o

Wed, 5 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

HAKUNA kama Samuel Eto’o kwa ufungaji mabao mengi katika historia ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON’, ambayo inatarajia kuanza Januari 9, hadi Februari 6 mwaka huu.

Gwiji huyo wa soka. raia huyo wa Cameroon amefunga mabao 18 katika fainali sita alizochezea timu ya Taifa ya nchi hiyo maarufu kama The Indomitable Lions.

Nyota huyo amepata kuchezea miamba mbalimbali ya Ulaya ikiwemo Real Madrid na Barcelona zote za Hispania, Inter Milan ya Italia na Chelsea ya England ameichezea Cameroon michezo 118, akifunga mabao 56 katika mashindano yote na kati ya hayo 18 ni fainali za AFCON.

Eto’o akiwa na rekodi ya mfungaji bora wa muda wote wa mashindano hayo, mbele ya mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Ivory Coast, Laurent Pokou mwenye magoli 14, alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Cameroon waliochukua ubingwa mara mbili mfululizo mwaka 2000 na 2002.

Pia alishiriki katika fainali za mwaka 2004, 2006, 2008 na 2010, akifunga bao karibu kila mashindano ikiwa pia ni rekodi sawa na Kalusha Bwalya wa Zambia na Asamoah Gyan wa Ghana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: