Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afisa LATRA aliemtishia dereva lori panga asimamishwa kazi (+video)

Video Archive
Tue, 17 Nov 2020 Chanzo: millardayo.com

Mamlaka ya Udhibiti usafiri Ardhini LATRA imemsimamisha kazi Afisa wake kutoka Mkoa wa Lindi ambaye video yake imesambaa mtandaoni akimshikia silaha aina ya panga dereva wa lori lenye namba ya usajili T412 DNN kilichotokea tarehe 11/11/2020.

Mkurugenzi Mkuu wa LATRA Gilliard Ngewe amesema sasa kinachoendelea ni uchunguzi wa tukio hilo na adhabu kali zitachukuliwa kwa muhusika ndani ya siku 21 za uchunguzi kulingana na sheria za utumishi wa umma.

“Hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria dhidi ya Afisa huyo zinaendelea kuchukuliwa na hatua ya kumsimamisha kazi imechukuliwa kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2003 ya utumishi wa umma” Mkurugenzi Mkuu LATRA

Chanzo: millardayo.com