Nchi

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuNchiPeopleBeauty
Wema Abraham Sepetu

Watu Maarufu Tanzania

Beauty

Wema Abraham Sepetu

Miss Tanzania 2006

Wema Sepetu
Tarehe ya Kuzaliwa:
1990-09-28
Mahali pa Kuzaliwa:
Tanzania

Wema Sepetu (amezaliwa 28 Septemba 1990) ni mwigizaji wa Tanzania na mshiriki wa urembo ambaye alishinda shindano la Miss Tanzania mnamo 2006. Aliiwakilisha Tanzania katika Miss World 2006, iliyofanyika Poland. Baadaye alikua mwigizaji nchini Tanzania.

Wema anatokea kwenye familia ya kidiplomasia ya Marehemu Balozi Abraham Sepetu. Ndiye mzaliwa wa mwisho katika familia ya watoto wanne. Alipata elimu yake ya msingi, na sekondari katika Shule Academic International School jijini Dar Es Salaam, Tanzania, na baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Teknolojia ya Ubunifu cha Limkokwing nchini Malaysia ili kufanya kozi ya biashara ya kimataifa ambayo alifanya kwa mwaka mmoja kisha akaacha endelea na uigizaji. Wema ameshawahi kutoka kimapenzi na mastaa kama Diamond Platinumz na mwigizaji Idris Sultan.Uigizaji

Aliingizwa kwenye tasnia ya sinema na marehemu Steven Kanumba wakati wa uchumba wao, alifanya filamu yake ya kwanza kwa jina la Apoint of no return akiigiza kama Dina akiwa mhusika mkuu pamoja na Steven Kanumba, aliigiza kama binti mdogo ambaye analazimishwa na familia yake kuolewa na Lameck (Steven Kanumba) aliekuwa mchawi na ambaye sio chaguo lake.

Baadaye alionekana kwenye sinema nyingi kama vile Family Tears, Red Valentine,White Maria ambazo zilimfanya kuwa mmoja wa waigizaji maarufu nchini Tanzania. Ameonekana katika filamu zaidi ya 20.

Mnamo mwaka 2011 alitengeneza sinema iitwayo Superstar, filamu ambayo inaelezea maisha yake ya kimahusiano na mwanamuziki Diamond Platnumz. Sinema hiyo ilizinduliwa mnamo mwaka 2012 katika Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar Es salaam na ilisifiwa na watu wengi akiwemo Omotola Jalade Ekeinde kutoka Nigeria ambaye alikuwa mgeni wa heshima.

Lakini sinema haikuingia sokoni hadi leo na Wema alisema kuwa bado anatafuta msambazaji bora ambaye anaweza kumlipa kulinganisha na gharama zake za uzalishaji kwani alisema kwamba wasambazaji wengi wameahidi pesa kidogo ikilinganishwa na kile alichowekeza. Baada ya hapo alionekana kwenye sinema kama Basilisa,It was not me, House boy, Madame kati ya nyingi.

Mnamo mwaka 2014 alishirikiana na Van Vicker kutoka nchini Ghana kutengeneza sinema iitwayo Day After Death wakiwa kama waigizaji wakuu. Filamu hiyo ilipangwa kutolewa mnamo mwaka 2015, lakini kutokana na ucheleweshaji haijaingia sokoni hadi leo, mbali na D.A.D kutoachiliwa.

Kwa bahati nzuri wakati wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ya miaka 30 alifanya uzinduzi wa sinema ya DAD na kuifanya kuwa sinema pendwa zaidi. Wema alionekana katika sinema zingine kutoka 2015-2016 kama vile Family, Mapenzi Yamerogwa and Chungu Cha Tatu kati ya nyingi.

Mnamo mwaka 2017 alirejea na filamu yake kwa jina la Heaven Sent, ambayo aliitengeneza na kuwa mhusika mwongozaji ambayo pia alikuwa na Salim Ahmed (Gabo) kama mhusika mkuu, uzinduzi huo ulifanyika Century Cinemax Mlimani City jijini Dar Es salaam nchini Tanzania. sinema iliuzwa kupitia programu yake ya rununu (simu) Wema App.

Filamu hii iliteuliwa katika vipengele saba (7) kwenye tukio la Sinema Zetu International Film Festival Awards 2018, pamoja na muigizaji Bora wa kike na Filamu Bora ya Kipindi, ambapo Wema alishinda Mwigizaji Bora wa kike na sinema ilishinda Chaguo la Watu.

Endeless Fame Production

Mnamo mwaka 2013 alizindua kampuni yake kwa jina la Endless Fame Production. Kampuni hiyo inahusika na utengenezaji wa sinema na Usimamizi wa wasanii, wameweza kusimamia baddhi ya wanamuziki wa Kitanzania kama vile Mirror na Ally Luna. Kampuni hiyo imetengeneza sinema kama vile Supestar, Unexpected, Day After Death, Family, and Heaven Sent.

Baadhi ya filamu za Wema House Boy Crazy Tenant Dj Ben Basilisa The Diary Lerato 14 Days Tafrani White Maria Sakata Red Valentine Family Tears A Point of No Return

Wikipedia